2023
Kuwa Mwenye Kujitegemea
Septemba 2023


Ujumbe wa Kiongozi wa Eneo

Kuwa Mwenye Kujitegemea

“Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi;… ”1 ndivyo Bwana alivyomwambia Adamu wakati alipomfukuza kutoka Bustani ya Edeni. Huo ulikuwa mwanzo wa kujitegemea, kama tunavyofahamu leo hii. Kujitegemea ni “uwezo, msimamo na juhudi ya kukidhi mahitaji ya kiroho na kimwili kwa ajili ya mtu binafsi na familia. Pale waumini wanapokuwa wenye kujitegemea, wanaweza pia kutumikia vyema na kuwajali wengine vyema,”2 na kazi inapewa heshima kama kanuni ya msingi katika maisha yao.

Tunapopiga hatua kuelekea kujitegemea, mara nyingi haitakuwa rahisi. Kutakuwepo vikwazo visivyoonekana na changamoto ambazo zitaingia kufanya iwe vigumu kufikia mafanikio. Hapo ndipo tunahitajika kukumbuka kwamba upinzani ni sehemu muhimu ya mpango wa wokovu. “Kwani lazima, kuwe na upinzani katika vitu vyote. Kama siyo hivyo … utakatifu haungepatikana, wala haki au hofu, wala uzuri au ubaya.”3

tunapokumbuka hilo, ndipo kisha tunaelewa kwamba sala kwa Baba yetu wa Mbinguni lazima iwe kipengele cha mlinganyo. Sala italeta nguvu wezeshi za upatanisho wa Mwokozi kuwa pamoja nasi, kutusaidia tuvuke na tuhimili majaribu au changamoto hizo ambazo hatuwezi kuzidhibiti. Nyingi nyakati zingine, zinaweza kuwa matokeo ya kuanguka kwetu wenyewe, utu wetu au tabia yetu au hata mtindo wa maisha. Tunapotafuta mwongozo na hakikisho kutoka Kwake, Yeye atatusaidia tuvunje vikwazo ili tufikie mafanikio ambayo tunayatamani katika utafutaji wetu.

Tunapaswa pia kukumbuka kwamba kufanya kazi kwa bidii, katika safari ya kuelekea kujitegemea si hitaji pekee. Tutahitaji kuvumilia hadi mwisho. Tutahitaji “subira ya Mungu ya kuvumilia yote, ambayo hutupatia nafasi za kujiboresha, kulingana na nafasi au muda wa kujiendeleza unaohitajika kwa dharura, kujitendea wenyewe”4 na, “kutosubiri kutendewa,”5 na kukuza kile kilichotolewa kwetu. Hatupaswi kukaa tu na kungojea mambo yawe. Hatupaswi kukaa tu na kulalamika kuhusu hali zetu mbaya au ngumu. Badala yake, kwa sala tumlilie Bwana kila siku ili atuoneshe wapi pa kupiga hatua inayofuata, na tusimame na twende na kutenda. Haitakuwa rahisi, lakini kidogo kidogo, kwa kuendelea kutenda, mambo yataanza kutukia. Bwana atatufungulia milango katika njia za kushangaza. Hilo litatokea ikiwa hatukati tamaa, bali tunaendelea kujaribu tena na tena.

Tunapofanya makosa njiani, kama ambavyo itakuwa mara nyingi, basi tusiruhusu makosa hayo yatuvunje. Tusisalimu amri kwenye kushindwa kwetu. Badala yake, tujifunze kutokana na kushindwa. Acha tujifunze kutokana na nyakati ngumu na kulingana na Mzee Joseph B. Wirthlin (1917–2008), “tuwe imara, wenye busara na wenye furaha kama matokeo.’’6 Anamaanisha kwamba taabu na huzuni hujaribu, huimarisha na hutakasa tabia yetu. Haiji kwa mtu mmoja pekee. Inakuja kwa wote. Lakini jinsi tunavyoishughulikia huamua vile matokeo yatakavyokuwa. Bwana huleta majaribu hayo kwenye maisha yetu ili kutufanya tujifunze masomo kutoka kwenye majaribu hayo.7

Rais Russell M Nelson, nabii, kwenye matukio zaidi ya mawili amefunza kwamba “Bwana anapenda juhudi.”8 Kwa hivyo, acha tuweke juhudi, kwenye kila tunachofanya, ikiwa tunataka kuwa wenye kujitegemea. Acha nipendekeze njia nne za jinsi tunavyoweza kufanya hili:

  1. Sala binafsi na ya familia kila siku –ili kuweka juhudi zetu katika sala, ili Bwana aweze kutuongoza ni uelekeo upi tuchukue na kipi tufanye na watu gani wa kuwafikia ambao wanaweza kutusaidia kwenye mchakato.

  2. BYU Pathway Connect –jiunge na kozi sasa. Weka juhudi katika kutafuta jinsi ya kujiunga, kutoka kwa Askofu wako au Rais wako wa Tawi na nyenzo zinazohitajika na kisha soma na ujifunze. Haitakuwa rahisi, lakini pambana wakati ukitafuta msaada kutoka kwa marafiki na viongozi wengine.

  3. Kuwa na msimamo na vumilia hadi mwisho –mambo yatafanya kazi hatua kwa hatua ikiwa umefokasi kwenye ndoto zako. Kamwe hutojutia kwa kufanya uamuzi na kuweka juhudi za kusoma au kuwa na msimamo katika kufanya kazi kila siku.

  4. Usiogope –kuwa na imani – Rais Nelson amefunza kwamba, “Imani ni kinyume cha woga”.9 Songa kwa imani katika Bwana Yesu Kristo. Tunasoma pia kwenye maandiko kwamba, “kwani hofu ni ya shetani.” Ondoa hofu kwenye njia yako, kupitia sala. Usiogope kufanya mambo magumu, alimradi una mapenzi katika mambo hayo. Tunahitaji kukumbuka kwamba ikiwa tutafanya mambo rahisi leo, tutahitajika kufanya mambo magumu baadaye, lakini kinyume chake, ikiwa tutafanya mambo magumu leo, siku zetu za baadaye zina uwezekano mkubwa wa kuwa angavu na rahisi.

Ndiyo, tunahitaji kukumbuka kwamba tunapanda mbegu leo, na hiyo itaamua ni kiasi gani tunavuna, wakati msimu utakapofika. Kwa hiyo, basi “tuingize “mundu” kwa nguvu zetu zote,10 ili mavuno yetu yaweze kuwa mazuri. Kumshirikisha Bwana Yesu Kristo katika mchakato huu. Mzee Clark G. Gilbert, Rais wa zamani wa BYU-Pathway Ulimwenguni kote, na Rais wa zamani wa BYU-Idaho, katika ibada yake alifundisha, “Yeye atakusaidia uvumilie kwa mapenzi katika malengo yako ya muda mrefu ya kuwa mkamilishaji.”11 Kwa hivyo endelea kwa ujasiri, ukijua kwamba Yeye anafahamu kila hitaji lako na atakusaidia.

Mzee Joseph B Wirthlin alitukumbusha kwamba Bwana Yesu Kristo ni mshirika, msaidizi na mtetezi wetu katika yote haya.12 Anataka tuwe na furaha. Anataka tufanikiwe. Ikiwa tutafanya sehemu yetu, Yeye ataingilia kati. Yeye aliyeshuka chini ya vitu vyote atakuja kutusaidia. Atatufariji na kutushikilia. Atatuimarisha katika udhaifu wetu na kutuwekea ngome katika taabu zetu. Atafanya mambo dhaifu yawe yenye nguvu. Yote tunayohitajika kufanya ni kusali kisha kufanya kadiri tuwezavyo, kwa uwezo wetu wote kila siku. Yanayobaki yaweke mikononi Mwake. Katika jina la Yesu Kristo. Amina.

Tanbihi

  1. Mwanzo Sura ya 3:19.

  2. Kitabu cha Maelezo – Kusimamia Kanisa, 22.0, Maktaba ya Injili.

  3. 2 Nefi 2:11.

  4. Neal A. Maxwell, “Endure It Well,” Ensign, May 1990, 33.

  5. Ona 2 Nefi 2:26.

  6. Joseph B. Wirthlin, “Come What May and Love It,” Liahona, Nov. 2008, 26.

  7. Ona Neal A. Maxwell, “Vumilia Vyema,” 33.

  8. Katika Joy D. Jones, “Wito Uliotukuka Hasa,” Liahona, Mei 2020, 16.

  9. Russell M. Nelson, “Let Your Faith Show,” Liahona, May 2014, 29.

  10. Ona Mafundisho na Maagano 4:4; 6:3; 11:3; 12:3; 14:3.

  11. Clark G. Gilbert, “From Grit to Grace” [BYU-Pathway Worldwide Devotional Speeches, Sept. 25, 2018], byupathway.org/speeches.

  12. Ona Joseph B. Wirthlin, “Come What May and Love It,” 28.