2023
Uhusiano kati ya Nyumbani na Kanisa
Septemba 2023


Handbook Highlight

Uhusiano kati ya Nyumbani na Kanisa

Kazi ya wokovu na kuinuliwa kitovu chake ni nyumbani na kusaidiwa na Kanisa. Kanuni zifuatazo zinatumika katika uhusiano kati ya Nyumbani na Kanisa.

  • Viongozi na walimu waheshimu wajibu wa wazazi na kuwasaidia. Viongozi na walimu waanzishe na kudumisha mawasiliano yenye tija na wazazi.

  • Viongozi watafute kuhakikisha kwamba mikutano ya Kanisa, shughuli, na mipango inasaidia watu binafsi na familia katika kufanya kazi ya wokovu na kuinuliwa katika nyumba zao.

  • Baadhi ya mikutano ya Kanisa ni muhimu katika kila kata au tawi. Hii inajumuisha mikutano ya sakramenti na madarasa na mikutano ya akidi inayofanywa siku ya Sabato. Mikutano mingine mingi, shughuli, na programu sio muhimu. Viongozi waipange kama itavyohitajika ili kukidhi mahitaji ya watu binafsi na familia. Viongozi wazingatie hali ya mahali husika na rasilimali.

  • Watu binafsi na familia wafikirie hali zao wakati wanapofanya maamuzi kuhusu kushiriki katika programu za Kanisa ambazo si za lazima.

  • Huduma za Kanisa na ushiriki zinahitaji kipimo cha dhabihu. Bwana atawabariki waumini wanapohudumu na kutoa dhabihu katika Kanisa Lake. Hata hivyo, kiasi cha muda kilichotengwa kwa ajili ya huduma ya Kanisa hakipaswi kupunguza uwezo wa waumini kukamilisha wajibu wao nyumbani, kazini, na sehemu nyingine. Viongozi na waumini hawapaswi kuzidiwa na wajibu mwingi wa Kanisa. Wala hawapaswi kutakiwa kufanya dhabihu za ziada ili kusaidia mipango au shughuli za Kanisa.

Kadiri waumini watakavyofuata kanuni hizi na misukumo ya Roho, Baba wa Mbinguni atabariki juhudi zao.

(Chanzo: Kitabu cha Maelezo ya Jumla, sehemu ya 2.3)