Miaka 100 ya Jioni ya Familia Nyumbani
Mwezi huu unaadhimisha miaka 100 tangu Urais wa Kwanza uwahimize waumini kuwa na jioni ya familia nyumbani. Dondoo zifuatazo zinatoka katika barua ya Urais wa Kwanza ukiitambulisha jioni ya familia nyumbani. Ilitolewa Aprili 1915 na kuchapishwa katika Improvement Era Juni 1915 (Kurasa 733–34). Herufi kubwa na vituo vmefanywa kuwa vya kisasa.
Wapendwa Kaka na dada zangu:
Tunawashauri Watakatifu wa Siku za Mwisho kuzingatia zaidi amri ya Bwana iliyotolewa katika sehemu ya 68 ya Mafundisho na Maagano:
“Na tena, ili mradi wazazi wanao watoto katika Sayuni, au katika kigingi chake chochote ambacho kimeundwa, ambao hawawafundishi wao kuelewa mafundisho ya toba, imani katika Kristo Mwana wa Mungu aliye hai, na ubatizo na kipawa cha Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono, wafikapo miaka minane, dhambi zao zitakuwa juu ya vichwa vya wazazi ; …
Na pia wawafundishe watoto wao kuomba, na kusimama wima mbele za Bwana” [ona M&M 68:25–28].
Watoto wa Sayuni wanapaswa pia kushika kwa ukamilifu zaidi amri ambayo Bwana alitoa kwa Israeli ya kale na kuirudia kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho.
“Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako” [Kutoka 20:12].
Funuo hizi zinatumika kwa nguvu zaidi kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho na inahitajika kwa akina baba na akina mama katika Kanisa hili kuwa amri hizi zifundishwe na kutumiwa majumbani mwao.
Kwa hivyo, tunawashauri na kuhimiza uanzishwaji wa “jioni ya familia nyumbani” Kote katika Kanisa ambapo akina baba na mama wanaweza kuwakusanyika wavulana na wasichana wao nyumbani na kuwafundisha neno la Bwana. Wanaweza basi kujifunza kikamilifu zaidi mahitaji na matakwa ya familia zao, wakati huo huo wakifahamiana wao kwa wao na watoto wao kwa undani zaidi pamoja na kanuni za injili ya Yesu Kristo. Jioni hii ya nyumbani inapaswa kutengwa kwa ajili ya sala, kuimba nyimbo za dini, nyimbo, muziki wa vyombo, kusoma maandiko, mada za familia na mafunzo mahususi ya kanuni za injili na matatizo ya kimaadili ya maisha, pamoja na majukumu ya watoto kwa wazazi, nyumba, Kanisa, jamii na taifa. Kwa watoto wadogo, ukariri sahihi wa, nyimbo, hadithi na michezo inaweza kuanzishwa. Viburudisho vyepesi ya aina hiyo kwa kiwango kikubwa vilivyotengenezwa nyumbani vinaweza kuandaliwa.
Urasmi na ugumu unapaswa kuepukwa kabisa na familia nzima inapaswa kushiriki katika mazoezi haya.
Mikusanyiko hii itatoa fursa za maelewano na kuaminiana kati ya wazazi na watoto, kati ya kaka na dada, na pia kutoa nafasi kwa maneno ya kuonya, ushauri na mwongozo kutoka kwa wazazi kwa ajili ya wavulana na wasichana wao. Itatoa fursa kwa wavulana na wasichana kuwaheshimu baba na mama zao na kuonyesha shukrani yao kwa baraka za nyumbani ili ahadi za Bwana kwao ziweze kutimia kihalisi, na maisha yao kurefushwa na kufanywa kuwa ya furaha. …
Tunawahimiza vijana kubaki nyumbani jioni hiyo na kutumia nguvu zao katika kuifanya kuwa yenye mafunzo, yenye faida, na ya kuchangamsha.
Ikiwa Watakatifu watatii ushauri huu, tunaahidi kuwa baraka kuu zitatokea. Upendo nyumbani na utiifu kwa wazazi utaongezeka. Imani itajengwa katika mioyo ya vijana wa Israeli, na watapata uwezo wa kupigana na vishawishi viovu na majaribu yanayowazonga.
Ndugu zenu,
Joseph F. Smith
Anthon H. Lund
Charles W. Penrose
Urais wa Kwanza