Si Dhambi Kuwa MDhaifu
Mwandishi anaishi Utah, Marekani.
Udhaifu na mapungufu si dhambi na hayawezi kutuzuia kuwa safi na wenye kustahili kuwa na Roho wa Mungu.
“Je ni kweli ninastahili kuingia katika nyumba ya Mungu? Je ninawezaje kuwa kama mimi si mkamilifu?”
“Je, Mungu anaweza kufanya udhaifu wangu kuwa nguvu? Nimefunga na kusali kwa siku nyingi ili tatizo hili liondolewe kutoka kwangu, lakini hakuna dalili ya mabadiliko.”
“Katika uwanja wa misheni niliishi injili kwa msimamo zaidi kuliko wakati wowote katika maisha yangu, lakini sijawahi kuwa na ufahamu wa mapungufu yangu. Kwa nini, wakati nilikuwa mzuri sana, nilikuwa najisikia vibaya wakati mwingine?”
Tukitafakari maswali kam hayo, ni muhimu kuelewa kwamba wakati dhambi ni dhahiri inatuongoza mbali na Mungu, udhaifu, kinyume chake unaweza kutuongoza kuelekea Kwake.
Kutofautisha kati ya dhambi na Udhaifu
Kwa kawaida tunafikiria dhambi na udhaifu kama tu alama nyeusi zenye ukubwa tofauti kwenye kitambaa cha roho zetu, uvunjaji sheria wenye uzito tofauti. Lakini maandiko yanasema kwamba dhambi na udhaifu ni urithi ulio tofauti, vinahitaji tiba tofauti, na vina uwezo wa kuzalisha matokeo tofauti.
Wengi wetu tuna uzoefu na dhambi kuliko tunavyojali kukubali, lakini hebu tupitie upya: Dhambi ni uchaguzi wa kutotii amri za Mungu au uasi dhidi ya Mwanga wa Kristo ndani yetu. Dhambi ni uchaguzi wa kumwamini Shetani zaidi kuliko Mungu, hutuweka katika uadui na Baba yetu. Tofauti na sisi, Yesu Kristo alikuwa hana dhambi kabisa na aliweza kulipia dhambi zetu. Wakati tunapotubu kwa dhati—pamoja na kubadilisha akili , moyo na tabia zetu; na kuomba msamaha sahihi au maungamo, tufanye malipo pale inapowezekana, na kutorudia dhambi hiyo siku zijazo—tunaweza kupata Upatanisho wa Yesu Kristo, kusamehewa na Mungu, na kuwa safi tena.
Kuwa safi ni muhimu kwa sababu hakuna kichafu kinachoweza kukaa katika uwepo wa Mungu. Lakini kama lengo letu tu ni kuwa bila hatia kama tulivyokuwa wakati tulipokuwa tunatoka katika uwepo wa Mungu, itakuwa bora zaidi kwetu sote kulala raha musterehe katika hori zetu kwa ajili ya mapumziko maisha yetu yote yaliyosalia. Badala yake, tulikuja duniani kujifunza kwa uzoefu ili kutofautisha mema na mabaya, kukua katika hekima na ujuzi, kuishi maadili ya maisha ambayo tunayajali, na kupata sifa ya utauwa—maendeleo ambayo hatuwezi kuyafanya kutokana na mipaka ya tenga la mtoto.
Udhaifu wa kibinadamu una jukumu muhimu katika madhumuni haya muhimu ya hapa duniani. Wakati Moroni alipokuwa na wasiwasi kwamba udhaifu wake wa maandishi ungesababisha watu wa mataifa mengine kudhihaki mambo matakatifu, Bwana alimhakikishia kwa maneno haya:
“Na ikiwa watu watakuja kwangu nitawaonyesha udhaifu wao. Nitawapatia watu udhaifu ili katika udhaifu wao wawe wanyenyekevu, na neema yangu inawatosha watu wote ambao hujinyenyekeza mbele yangu, kwa maana wakijinyenyekeza mbele yangu, na kuwa na imani ndani yangu, ndipo, nitafanya vitu dhaifu kuwa vya nguvu kwao” (Etheri 12:27; ona pia 1 Wakorintho 15:42–44; 2 Wakorintho 12:7–10; 2 Nefi 3:21; na Yakobo 4:7).
Maana ya andiko hili inajulikana ni muhimu sana na hutualika sisi kutofautisha dhambi (inayohimizwa na Shetani) na udhaifu (ilivyoelezwa hapa kama hali “tuliyopewa” na Mungu).
Tunaweza kuelezea udhaifu kama kikwazo kwa hekima yetu, nguvu na utakatifu ambayo inakuja kwa kuwa binadamu. Kama binadamu tunazaliwa wanyonge na tegemezi, tukiwa na dosari mbalimbali za kimwili na kimaelekezo. Tumelelewa na kuzungukwa na binadamu wengine dhaifu, na mafundisho yao, mifano, na wanayotutendea yana dosari na hutuharibu wakati mwingine. Katika udhaifu wetu, hali yetu ya kibinadamu tunapatwa na magonjwa ya kimwili na hisia, njaa, na uchovu. Tunajifunza hisia za binadamu kama hasira, huzuni na hofu. Tumekosa hekima, ujuzi, uthabiti, na nguvu. Na tuko chini ya majaribu ya aina nyingi.
Ingawa alikuwa bila dhambi, Yesu Kristo alijiunga pamoja nasi kikamilifu katika hali dhaifu ya mauti (ona 2 Wakorintho 13:4). Alizaliwa kama mtoto mchanga mnyonge katika mwili unaoweza kufa na kulelewa na walezi ambao si wakamilifu. Alikuwa ajifunze jinsi ya kutembea, kuzungumza, kufanya kazi, na kupatana vyema na watu wengine. Alipata njaa na uchovu, alihisi hisia za kibinadamu, na angeweza kuwa mgonjwa, kuteseka, kutokwa na damu, na kufa. Alikuwa “katika kila hali mwenye kujaribiwa kama sisi, bado hakuwa na dhambi,” alijikabidhi mwenyewe kwenye umauti ili aweze “kuguswa na hisia ya upungufu wetu” na kutusaidia katika upungufu wetu au udhaifu wetu (Hebrews 4:15; ona pia Alma 7:11–12).
Hatuwezi tu kutubu kwa kuwa ni wadhaifu—wala udhaifu wenyewe hautufanyi sisi kuwa wachafu. Hatuwezi kukua kiroho isipokuwa tukatae dhambi, lakini pia hatuwezi kukua kiroho isipokuwa tukubali hali yetu ya udhaifu wa kibinadamu, kujibu kwa unyenyekevu na kwa imani, na kujifunza kupitia udhaifu wetu kumwamini Mungu. Wakati Moroni alipokuwa na wasi wasi kuhusu udhaifu wa maandishi yake, Mungu hakumuambia atubu. Badala yake, Bwana alimfundisha kuwa mnyenyekevu na kuwa na imani katika Kristo. Tunapokuwa wapole na waaminifu, Mungu hutoa neema—si msamaha—kama dawa ya udhaifu. Kamusi ya Biblia inaeleza neema kama nguvu yenye kutuwezesha itokayo kwa Mungu ili tuweze kufanya kile ambacho hatuwezi kujifanyia wenyewe (tazama kamusi ya Bibilia, “Neema”)—tiba sahihi ya kiungu ambayo kwayo anaweza kufanya “vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu.”
Kutumia Unyenyekevu na Imani
Kutoka mapema katika uzoefu wetu Kanisani, tunafundishwa mambo muhimu ya toba, lakini jinsi gani hasa tunaweza kuendeleza unyenyekevu na imani? Zingatia yafuatayo:
-
Tafakari na kusali. Kwa sababu sisi ni wadhaifu, inawezakana tukakosa kutambua kama tunashughulika na dhambi (wito wa haraka ni kuenea kwa mabadiliko ya mawazo, moyo, na tabia) au udhaifu (wito wa unyenyekevu, juhudi endelevu, kujifunza, na kuboresha). Jinsi gani tunavyoangalia mambo haya inaweza kutegemea malezi na ukomavu wetu. Kunaweza hata kuwa na mambo yote mawili ya dhambi na udhaifu katika tabia moja. Kusema dhambi hakika kuwa ni udhaifu hutuongoza kwenye urazinishaji badala ya kutubu. Kusema udhaifu ni dhambi inaweza kusababisha aibu, lawama, kukata tamaa, na kukata tamaa katika ahadi za Mungu. Kutafakari na kusali kunatusaidia kubainisha tofauti hizi.
-
Weka kipaumbele. Kwa sababu sisi ni wadhaifu, hatuwezi kufanya mabadiliko yote mara moja. Tunaponyenyekea na kuamini kukabiliana na udhaifu wetu wa kibinadamu masuala machache kwa wakati mmoja, tunaweza kupunguza ujinga hatua kwa hatua, kuunda sampuli nzuri ya mazoea, kuongeza afya yetu ya kimwili na kihisia na uthabiti, na kuimarisha imani yetu katika Bwana. Mungu anaweza kutusaidia kujua wapi pa kuanzia.
-
Mpango. Kwa sababu sisi ni wadhaifu, kuimarika kutahitaji zaidi ya hamu ya haki na nidhamu nyingi. Sisi pia tuna haja ya kupanga, kujifunza kutokana na makosa, kuendeleza mikakati madhubuti zaidi, kurekebisha mipango yetu, na kujaribu tena. Tunahitaji msaada kutoka katika maandiko matakatifu, vitabu muhimu, na watu wengine. Tunaanzia kidogo, kufurahi katika kuboresha, na kuchukua tahadhari (hata ingawa kunatufanya kujihisi tunaweza kuathirika na wadhaifu). Tunahitaji msaada ili kutusaidia kufanya maamuzi mazuri hata wakati tunapokuwa na uchovu au tumekata tamaa na mipango ya kuturudisha katika njia sahihi tunapokuwa tumeteleza.
-
Tumia subira. Kwa sababu ya udhaidfu wetu, mabadiliko yanaweza kuchukua muda. Hatuachi tu udhaifu wetu kwa njia ile tunavyoacha dhambi. Wanafunzi wanyenyekevu hufanya kinachohitajika kwa hiari, kujifunza ujasiri, kuendelea kujaribu, na hawakati tamaa. Unyenyekevu unatusaidia kuwa na subira na sisi wenyewe na wengine ambao ni wadhaifu pia. Subira ni dhihirisho la imani yetu katika Bwana, shukrani kwa uaminifu Wake kwetu, na imani katika ahadi Zake.
Hata tunapotubu dhambi zetu kwa dhati, kupata msamaha, na kuwa wasafi tena, bado tunabaki wadhaifu. Bado tuko chini ya magonjwa, hisia, ujinga, maelekezo, uchovu, na vishawishi. Lakini udhaifu na mapungufu si dhambi na haviwezi kutuzuia kuwa wasafi na wenye kustahili kuwa na Roho wa Mungu.
Udhaifu kuwa Nguvu
Wakati Shetani ana nia ya kutumia udhaifu wetu kutushawishi katika dhambi, Mungu anaweza kutumia udhaifu wa binadamu ili kufundisha, kuimarisha, na kutubariki. Kinyume na kile tunachoweza kutarajia au kutumaini, hata hivyo, Mungu si daima, “hufanya vitu dhaifu kuwa imara” kwetu kwa kuondoa udhaifu wetu. Wakati Mtume Paulo alipoomba kwa Mungu mara kadhaa kuwa amuondolee “mwiba katika mwili” Shetani alitumia kipigo chake, Mungu alimwambia Paulo, “Neema yangu inakutosha wewe; maana uwezo wangu hukamilishwa zaidi katika udhaifu” (2 Wakorintho 12:7, 9).
Kuna njia nyingi Bwana hufanya “vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu.” Wakati Yeye anaweza kuondoa udhaifu kupitia tiba ya kiajabu tunayotumaini, lakin katika uzoefu wangu binafsi hii kwa kiasi fulani ni nadra. Kwa mfano, naona hakuna ushahidi kwamba Mungu alimwondolea Moroni udhaifu wake wa kuandika baada ya aya maarufu katika Etheri 12. Mungu anaweza pia kufanya vitu dhaifu kuwa na nguvu na kutusaidia kufanya kazi licha ya udhaifu wetu, kupata hisia sahihi ya ucheshi au mtazamo juu ya hilo, na kuboresha hatua kwa hatua baada ya muda. Pia, uwezo na udhaifu mara nyingi huhusiana (kama nguvu ya uvumilivu na udhaifu wa ukakamavu), na tunaweza kujifunza kuthamini nguvu na udhaifu wa hasira ambao huendana nayo.
Kuna njia nyingine ambayo ina nguvu zaidi ambayo Mungu hufanya mambo dhaifu kuwa na nguvu kwetu. Bwana anasema na Moroni katika Etheri 12:37, “Kwa sababu umeuona udhaifu wako, utafanywa kuwa mwenye nguvu, hata kukaa mahali nimepatayarisha katika nyumba ya Baba yangu.”
Hapa Mungu haahidi kubadili udhaifu wa Moroni, lakini kumbadili Moroni. Kwa kukabiliana na changamoto ya udhaifu wa kibinadamu, Moroni—pamoja na sisi—tunaweza kujifunza wema, huruma, upole, uvumilivu, ujasiri, kutokata tamaa, hekima, uthabiti, msamaha, ukakamavu, shukrani, ubunifu, na mengineyo ambayo hutufanya kuwa zaidi kama Baba yetu wa Mbinguni. Hizi ndio sifa hasa tulizokuja duniani kujifunza, sifa za Kikristo ambazo zinatuandaa ili turudi nyumbani hapo juu.
Hakuna mahali popote upendo wa Mungu, hekima, na nguvu ya ukombozi ni dhahiri zaidi kuliko uwezo Wake wa kubadilisha shida zetu na udhaifu wa binadamu katika fadhila za kiungu na uwezo wa kutufanya kuwa zaidi kama Yeye.