“Katika masomo yote tunayojifunza kutoka katika maisha ya Mwokozi, hakuna kilicho wazi na chenye nguvu zaidi ya somo la utii,” alifundisha Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili katika mkutano mkuu wa Aprili 2014. Mfano wa Mwokozi unatufundisha siyo tu kwa nini utiifu kwa Baba wa Mbinguni ni muhimu lakini pia ni jinsi gani tunaweza kuwa watiifu. Unapopitia upya mifano ifuatayo toka kwenye utumishi Wake, fikiria jinsi unavyoweza kutengeneza njia kwa ajili ya kuifuata katika maisha yako.
1. Japokuwa Yesu hakuwa na dhambi, alikubali ubatizo “ili kutimiza haki yote” (Mathayo 3:13–17 ; onapia 2 Nefi 31:4–7 ; Yohana 3:5 ).
2. Akiwa na umri wa miaka 12, wakati Joseph na Mary walipompata Yesu akifundisha hekaluni, Aliwatii wao, “na kwa utiifu alirudi nyumbani pamoja nao” (ona Luka 2:42–51 ).
3. Japokuwa Aliomba kama kikombe kingemwepuka, Alijitoa na kuteseka katika Bustani ya Gethsemen (ona Mathayo 26:36–44 ; Luka 22:39–54 ).
4. Aliitii siku ya Sabato na alihudhuria ibada katika sinagogi (ona Luke 4:16–44 ).
5. Yesu alijitoa ili ahukumiwe na wanadamu ili kazi ya Bwana na utukufu uweze kukamilika (ona Isaya 53:7 ; Mathayo 26:53 ; Musa 1:39 ).
6. Alimaliza kazi yake kwa kuruhusu watu waovu kumsulubisha Yeye (ona Mathayo 27:35 ; Yohana 10:17–18 ; Wagalatia 1:3–5 ).
7. Wakati wote akiwa mtiifu kwa Baba Yake, Yesu alienda kwenye ulimwengu wa roho na kuanzisha kazi ya umisionari kule (ona 1 Petro 3:18–20 ; 4:6 ).
8. Yesu alijaribiwa na Shetani, lakini hakushindwa (ona Mathayo 4:1–11 ; M&M 20:22 ).
9. Aliendelea kufanya mapenzi ya Bwana na kuliongoza Kanisa (ona Joseph Smith—Historia 1:16–17 ; M&M 19:2, 24 ).
Mzee Hales alisema, “Yesu alifundisha kutii katika lugha rahisi ambayo ni rahisi kuielewa: ‘Kama unanipenda, tii amri zangu’ [Yohana 14:15 ], na ‘Njoo, unifuate’ [Luka 18:22 ].” Utafanya nini leo ili kuwa mtiifu zaidi?
“Kwa sababu Mwokozi wetu alikuwa mtiifu, Alilipia dhambi zetu, kufanya uwezekano wa ufufuko wetu na kuandaa njia kwaajili yetu kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni, ambaye alijua tungefanya makosa wakati tukijifunza utii katika maisha ya mwili wa kufa. Tunapotii, tunakubali dhabihu Yake, kwani tunaamini kwamba kupitia Upatanishi wa Yesu Kristo, watu wote wanaweza kuokolewa, kwa utiifu wa sheria, ibada, na amri zilizotolewa katika injili.”
Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, “‘Kama Unanipenda, Shika Amri Zangu,’” Liahona, Mei 2014, 35.