2015
Dini Safi
Aprili 2015


Dini Safi

Huduma isiyo na uchoyo—kujisahau wenyewe, kutatua na shida za wengine, na kuweka chini maisha yetu katika huduma yao—imekuwa tabia ya wafuasi wa Yesu Kristo.

composite of different families

Vielelezo na Annie Henrie

Katika Mathayo sura ya 11 Mwokozi anatufundisha somo muhimu kwa kile alichokifanya si kusema katika jibu la swali lililoulizwa na wafuasi wa Yohana Mbatizaji:

“Sasa wakati Yohana aliposikia akiwa gerezani habari ya matendo ya Kristo, aliwatuma wanafunzi wake wawili,

Na akamwambia, wewe ni yule anayekuja, au tumngoje mwingine?

Yesu akajibu na akawaambia, Nendeni na umwonyeshe tena Yohana yale ambayo mumesikia na kuyaona:

Vipofu wanapata kuona, viwete watembea, wenye ukoma wanatakaswa, na viziwi wasikia, wafu wafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema” (Mathayo 11:2–5).

Badala ya kutoa mafundisho mafupi ya maelezo na kuelezea kwamba Yeye alikuwa, kwa kweli, “ndiwe yule ajaye,” Mwokozi alijibu kwa njia ya yale anayofanya—mfano Wake wa huduma.

Katika mkutano mkuu wa Aprili, 2014 Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitukumbusha: “Tunamtumikia Baba yetu wa Mbinguni kwa haki kwa kushawishi wengine na kuwahudumia. Mfano mkubwa wa aliyewahi kutembea ulimwenguni ni Mwokozi wetu, Yesu Kristo.”1

Huduma isiyo na uchoyo—kujisahau wenyewe, kuta tua na shida za wengine, na kuweka chini maisha yetu katika kuwahudumia wao—daima ni tabia ya wanafunzi wa Yesu Kristo. Kama Mfalme Benjamin alivyofundisha zaidi ya miaka 100 kabla ya kuzaliwa kwa Mwokozi, “Na tazama nawaambia vitu hivi ili mpate hekima ili mjifunze kwamba mnapowatumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu” (Mosia 2:17).

Yakobo anatukumbusha kipengele muhimu cha “dini safi” hupatikana katika huduma yetu kwa wengine kama “kuwatembelea yatima na wajane katika shida zao” (Yakobo 1:27). “Dini safi” ni zaidi ya tamko la imani; ni maonyesho ya imani.

Wapende wasafiri wenzako

Katikati ya Julai 1984, wiki kadhaa tu baada ya mke wangu, Carol, na mimi kufunga ndoa katika Hekalu la Los Angeles California, tulikuwa njiani tukielekea Utah, mahali ambapo ningeeanza kazi yangu na Carol angemaliza masomo yake katika chuo kikuu. Tulikuwa tunaendesha magari tofauti. Kati ya magari haya mawili, tulikuwa tukisafirisha kila kitu tulichomiliki.

Kama nusu ya safari yetu, Carol alisogea kando ya gari langu na kuniashiria nisimame. Hii ilikuwa katika siku zile kabla ya simu za mkononi na smartfoni, ujumbe mfupi wa simu na Twita. Baada ya kuona ishara katika uso yake kupitia dirisha la gari lake, niliweza kutambua hakuwa anajisikia vizuri. Aliwasiliana nami kwamba anaweza kuendelea kuendesha gari, lakini nilikuwa na wasiwasi kwa ajili ya mke wangu tuliyefunga ndoaa hivi karibuni.

Tulipokaribia mji mdogo wa Beaver, Utah, alisogea kando ya gari langu tena, na nilijua kwamba alihitaji kusimama. Alikuwa mgonjwa na hakuweza kuendelea. Tulikuwa na magari mawili yaliyojaa nguo na zawadi za harusi, lakini kwa bahati mbaya tulikuwa na fedha kidogo. Chumba cha hoteli kilikuwa nje ya bajeti yetu. Sikuwa na uhakika na cha kufanya.

Hakuna aliyewahi kufika Beaver kati yetu, na sikuwa na uhakika nilikuwa natafuta nini, tuliendesha tukizunguka kwa dakika chache hadi nikaona bustani. Tuliingia ndani ya bustani hiyo na tuliona mti ulio na kivuli kidogo, ambapo nilitandika blanketi ili Carol aweze kupumzika.

Dakika chache baadaye gari nyingine iliingia katika bustani hiyo na kuegesha gari hilo karibu na magari yetu mawili. Mwanamke, wa umri wa mama zetu, alitoka nje ya gari yake na kutuuliza kama kulikuwa na shida na kama angeweza kutusaidia. Alisema alikuwa ametutambua alipokuwa akitupita na alihisi kuwa alipaswa kusimama. Wakati tulipomwelezea hali yetu, mara hiyo alitualika nyumbani kwake, ambapo tungepumzika kwa muda tuliotaka.

Punde tulijikuta juu ya kitanda kizuri katika chumba chake cha kulala kilichokuwa chini ya nyumba yake na chenye baridi kidogo. Punde tulipotulia, dada huyu mzuri alitueleza kuwa alikuwa na shughuli kadhaa za kufanya na kwamba tungeachwa pekee yetu kwa saa chache. Alituambia kwamba kama tutasikia njaa, tulikuwa tumekaribishwa kwa kitu chochote tulichoweza kupata jikoni, na kama tungeoondoka kabla ya yeye kurudi nyumbani, tafadhali tungemfungia mlango wa mbele.

Baada ya kupata usingizi wa kutosha, Carol aliona ilikuwa vyema tuendelee na safari yetu bila kuenda jikoni. Wakati tulipoondoka, huyo mwanamke mkarimu hakuwa amerudi nyumbani kwake. Kulingana na kumbukumbu yetu, hatukuandika anwani na kamwe hatukumshukuru huyo msamaria mwema, ambaye alisimama njiani na kuwafungulia nyumba yake wageni walio kuwa na shida.

Nikitafakari juu ya tukio hilo, maneno ya Rais Thomas S. Monson, ambaye anajumuisha mawaidha ya Mwokozi na “enenda zako nawe ukafanye vivyo hivyo” (ona Luka 10:37) kama vile binadamu katika akili yake: “Hatuwezi kwa kweli kumpenda Mungu kama hatuwezi kupenda wasafiri wenzetu katika safari hii ya mauti.”2

Popote tunapokutana na “wasafiri wenzetu”—kwenye barabara au kwenye nyumba zetu, kwenye uwanja wa michezo au katika shule zetu, kazini au kanisani—tunapotafuta, kuona, na kutenda, tutakuwa kama Mwokozi, tukibariki na kuhudumia njiani.

Tafuta

drawing of woman praying

Vielelezo na Annie Henrie

Mzee Neal A. Maxwell (1926–2004) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifunza:

“Tofauti na Mwokozi wetu, hakika sisi hatuwezi kufidia dhambi za wanadamu! Aidha, kwa hakika hatuwezi kubeba magonjwa yote ya binadamu, udhaifu, na masikitiko (ona Alma 7:11–12).

“Hata hivyo, kwa kipimo chetu kidogo, kama vile Yesu alivyotualika, tunaweza kujitahidi kuwa ‘hata kama [vile Yeye alivyo]’ (3 Nefi 27:27).”3

Tunapotafuta kuwa kama Yeye, tukiwa na hamu ya dhati ya kubariki “wasafiri wenzetu,” tutapatiwa fursa kusahau ubinafsi wetu na kuwainua wengine. Fursa hizi mara nyingi huwa si rahisi, kupima hamu yetu ya kweli ya kuwa kama Bwana, ambaye huduma yake ndio kubwa ya zote, Upatanisho Wake usio na mipaka, ni kitu chochote bali rahisi. Hata hivyo, Yeye anasema, “utukufu na uwe kwa Baba, na Mimi nikachukua na kukamilisha maandalizi yangu kwa wanadamu” (M&M 19:19).

Kutafuta kwa dhati kuwa kama Mwokozi itaturuhusu kuona kile ambacho hatungeweza kukiona vingenevyo. Msamaria wetu mwema aliishi karibu sana na Roho Mtakatifu na hivyo kumwezesha kujibu maongozi ya Mungu na kuweza kumkaribia mgeni aliyekuwa na shida.

Ona

drawing of three children with lantern

Vielelezo na Annie Henrie

Kuona kwa macho ya kiroho ni kuona vitu kama vile vilivyo kweli na kutambua shida ambazo vinginevyo hatungeweza kuzitambua. Katika fumbo la kondoo na mbuzi, si wale waliokuwa wamebarikiwa wala wale waliokuwa wamelaaniwa walikuwa wamemtambua Mwokozi katika wale walio kuwa na njaa, kiu, uchi, au gerezani. Waliyapo kea malipo yao kwa kuuliza, “Ni lini tulikuona ukiwa”? (Ona Mathayo 25:34–44).

Ni wale tu ambao walikuwa wameona kwa macho ya kiroho, na kutambua shida, walitenda na kuwabariki wale watesekao. Msamaria mwema wetu alitambua vile alivyoona kwa macho ya kiroho.

Tendo

drawing of older woman and young man

Vielelezo na Annie Henrie

Tunaweza kuona shida karibu nasi lakini tunaweza kuhisi kuwa duni kuitikia, tukidhania kwamba kile ambacho tunacho kitoa hakitoshelezi. Tunapotafuta kuwa hata kama Yeye na tunapoona mahitaji kwa wasafiri wenzetu kupitia macho ya kiroho, ni lazima tuamini kwamba Bwana anaweza kufanya kazi kupitia kwetu, na kisha ni lazima tuchukue hatua.

Walipokuwa wanaingia hekaluni, Petro na Yohana walikutana na mtu “kiwete tangu tumboni mwa mama yake” ambaye aliwaomba wampe sadaka (ona Matendo ya Mitume 3:1–3). Jibu la Petro ni mfano na mwaliko kwa kila mmoja wetu:

“Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende”.

Akamshika mkono wa kuume, akamwinua” (Matendo ya Mitume 3:6–7).

Tunaweza kutenda kwa kutoa wakati wetu na vipaji vyetu, neno la ukarimu, au mgongo imara. Tunapotafuta na kuona, tutawekwa katika mazingira na hali ambayo tunaweza kutenda na kubariki. Msamaria mwema alitenda. Alituchukua nyumbani kwake na kutupa kile alichokuwa nacho. Kimsingi yeye alisema, “Kile nilicho nacho ndicho nakupa.” Ilikuwa ndicho tulichohitaji hasa.

Rais Monson amefundisha kanuni sawa na hizo:

“Kila mmoja wetu, katika safari ya maisha ya duniani, atasafiri kwenye barabara yake ya Jericho mwenyewe. Je uzoefu wako utakuwa nini? Je wangu utakuwa nini? Je, nitashindwa kumtambua yule aliyeanguka miongoni mwa wezi na anahitaji msaada wangu? Je, wewe?

Je nitakuwa mmoja wa wale wenye kumtazama aliyejeruhiwa na kusikia ombi lake, lakini navuka upande mwingine? Je, wewe?

Au nitakuwa yule ambaye anaona, anasikia, anasimama, na kusaidia? Je wewe?

Yesu alitupa msemo wetu, ‘Nenda, nawe ukafanye vivyo hivyo.’ Tunapotii tamko hili, kunafunguka kwa maoni yetu ya milele ono la furaha ambalo ni nadra kulingana na kamwe kuzidiwa.”4

Tunapokuwa zaidi kama Mwokozi kwa kutafuta, kuona, na kutenda, tutakuja kujua ukweli wa maneno haya ya Mfalme Benjamin: “Kwamba mnapowatumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu” (Mosia 2:17).

Muhtasari

  1. Richard G. Scott, “Nimewapa Mfano,” Liahona, Mei 2014, 35.

  2. Thomas S. Monson, “Upendo—Kiini cha Injili,” Liahona, Mei 2014, 91.

  3. Neal A. Maxwell, “Apply the Atoning Blood of Christ,” Ensign, Nov. 1997, 22.

  4. Thomas S. Monson, “Your Jericho Road,” Ensign, Mei 1977, 71.