Ni kiasi gani ushawishi unafanya Shetani awe na nguvu dhidi ya mawazo yangu?
Baba yetu wa mbinguni anahakikisha kwamba tuna uhuru wa kimaadili, uwezo wa kuchagua mema na mabaya. Hata tulazimisha kutenda mema, na ibilisi hata tulazimisha kutenda maovu (ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 214).
Hivyo, wakati inapokuja kwenye mawazo yako, ibilisi ana ushawishi pale tu unapokubali kujiweka kwake. Nabii Joseph Smith alisema, “Shetani hawezi kutupotosha kwa ulaghai wake pengine sisi katika mioyo yetu tukubali na kusalimu amri” (Mafundisho: Joseph Smith, 213). Pia alisema, “Ibilisi hana uwezo dhidi yetu ila ni pale tu tunapomruhusu” (214).
Kwa nyongeza, maandiko yanatuambia kwamba “hakuna mwingine yeyote isipokuwa Mungu ambaye anayajua mawazo yako na nia ya moyo wako” (M&M 6:16), Kwa hiyo shetani hawezi kwa hakika kujua nini unachofikiria. Anaweza tu kuleta majaribu na ulaghai. Lakini kama utachagua kuyafuata, anapata nguvu kubwa dhidi yako na majaribu yanakuwa ya nguvu. Kwa ishara ileile, kama unastahimili maovu na kuchagua mazuri, utaimarishwa na kubarikiwa.