Mawazo ya Jioni ya Familia Nyumbani
Toleo hili lina makala na shughuli ambazo zinaweza kutumika kwa ajili ya jioni ya familia nyumbani. Yafuatayo ni mawazo mawili.
“Nina Haja Nawe Kila Saa,” ukurasa wa 30: Kama vile maneno ya wimbo “Nina Haja Nawe Kila Saa” yalivyomsaidia Pak Mi-Jung kuamua kubatizwa, nyimbo zinaweza kuwa na athari kubwa katika maisha yetu. Fikiria juu ya wakati ambao maneno ya wimbo yamebariki maisha yako na uzingatie kuelezea uzoefu huo kwa familia yako. Alika kila mwana familia achague wimbo aupendao na aseme jinsi ambavyo umebariki maisha yake. Kisha imba kila wimbo na familia yako. (Unaweza kuzigawa ili lifanyike kwa wiki kadhaa.)
“Sala na Makanisa Makuu,” ukurasa wa 68: Baada ya kusoma hadithi hii, onyesha picha za makanisa tofauti ama taja makanisa tofauti katika mji wako na uongee kuhusu maswali haya na familia yako: Ni mambo gani ambayo unayo, yanafanana na ya dini zingine? Je Baba wa Mbinguni anahisi vipi kuhusu watoto Wake wote? Tunapaswa kuwatendea vipi watu ambao wana imani tofauti? Zingatia kutumiamakala “Weka usawa kati ya Ukweli na Uvumilivu” na Mzee Elder Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume kumi na Wawili (Liahona, Feb. 2013, 28–35) ili kusaidia kujibu maswali haya.