Vijana
Sarah wa Mtu Mwingine
Mwandishi anaishi Utah, Marekani.
Nilikuwa ninaona vigumu kutumia imani yangu kama jibu la swali rahisi kama vile “Kwa nini haunywi kahawa”? Katika siku za nyuma nilikuja na visingizio kama vile Ni chungu sana ama sipendi ladha yake.
Je, ni kwa nini nilikuwa naona aibu? Kwa nini nilikuwa na hofu sana kusimama kwa ajili ya kile nilichoamini? Nikitazama nyuma sasa, Sielewi hasa kile nilichohofia. Lakini ninakumbuka hasa wakati nilipokoma kujificha nyuma ya visingizio.
Siku moja katika darasa langu la Kiingereza la shule ya sekondari, mwalimu alitangaza kwamba tungekuwa tunatazama kipindi cha televisheni nilijua sikuwa ninapaswa kukitazama. Wakati wanafunzi wengine wakishangilia kwa furaha, mwana darasa mwenzangu Sarah aliinua mkono wake na kuomba kama angeweza kuondoka.
Wakati mwalimu alipomwuliza ni kwa nini, Sarah alijibu kwa kusema ukweli, “Kwa sababu mini ni Mmormoni na huwa sitazami sinema za lugha chafu.”
Ujasiri wake kusimama mbele ya darasa ulikuwa wa ajabu. Shukrani kwa Sarah, mimi pia nilisimama na kusubiri nje kwa dhamiri safi hadi sinema ikaisha.
Nilibadilishwa milele. Nilianza kuelezea imani yangu badala ya kuepuka mada hiyo. Na kwa sababu ya hayo, nilipata kujiamini na nilishiriki zaidi katika shughuli za Kanisa na shuleni.
Sikuwahi kumwaambia Sarah jinsi nilvyouthamini mfano wake, lakini ninajaribu kuiga mfano wake wa ujasiri. Sasa ninatambua kwamba kuwa muumini wa Kanisa la Mungu zuri na takatifu, hakika si jambo la kuonea aibu. Ninatumaini kwamba ninaweza, kupitia mfano wangu, kuwa Sarah wa mtu mwingine.