Jinsi ya kuwa na Hekima
Toka Chuo Kikuu cha Brigham Young–Idaho hotuba ya mahafali yaliyotolewa Aprili 10, 2009.
Katika taarifa za siku hizi za mawimbi, tunahitaji sana hekima—hekima za kutafakari na kutambua jinsi ya kuyatumia yale tunayojifunza.
Acha tukumbuke:
-
Lazima tutafute hekima.
-
Hekima ni kubwa na inakuja katika ukubwa na rangi tofauti.
-
Hekima iliyopatikana awali inaleta baraka kuu.
-
Hekima katika upande mmoja haiwezi kuhamishwa kwa mwingine.
-
Hekima ya ulimwengu, katika hali nyingi ni yenye thamani, ni ya thamani kuu inapotumika kuabudu na kumheshimu Mungu.
Maandiko yanaelezea aina mbili za hekima: hekima ya ulimwengu na hekima ya Mungu. Hekima ya ulimwengu ina mambo yote mazuri na mabaya. Katika maelezo ya giza nene, inaweza kuelezewa kama baadhi ya ukweli, uliochanganyika na akili na hila, ili kufanikisha ubinafsi au malengo maovu.
Kuna aina nyingine ya hekima ya ulimwengu ambayo haikaribii uovu. Hakika inawezekana. Hekima hii inapatikana kwa kupitia kujifunza, kufikiria, kuangalia, na kwa kazi ngumu. Ni yenye thamani kubwa na inasaidia katika mambo tunayoyafanya. Kwa watu wazuri na wenye heshima, inakuja kama ilivyokuwa kwa mwili wetu wa kufa.
Muhimu zaidi, hekima inayoleta mafanikio katika ulimwengu lazima ikubali kurudi nyuma ya hekima ya Mungu na bila kufikiria kwamba inaweza kubadilishana nayo.
Siyo hekima zote zimeumbwa sawa. Tunahitaji kujifunza kwamba panapokuwepo na mvutano kati ya hekima ya ulimwengu na hekima ya Mungu, lazima tuelekeze mapenzi yetu kwenye hekima ya Mungu.
Ninashauri uchukue baadhi ya matatizo yanayo kukabili. Weka mstari katikati ya karatasi. Orodhesha hekima za ulimwengu upande wa kushoto na hekima za Mungu upande wa kulia. Andika vitu vyenye kupingana na vingine.
Ni chaguzi gani unazozifanya?
Katika sehemu ya 45 ya Mafundisho na Maagano, ambayo inaongelea matukio yanayo tuongoza kwenye Ujio wa Pili wa Mwokozi, Bwana tena anaelezea hadithi ya wanawali kumi na kisha akatuacha na maneno haya: “Kwani wale walio na hekima na kupokea ukweli, na kumchukua Roho Mtakatifu kuwa kiongozi wao, na hawajadanganywa—amini ninawaambia, hawatakatiliwa chini na kutupwa katika moto, bali watastahimili siku ile” (ona M&M 45:57).
Acheni tuitafute hekima ya Mungu. Kuna mengi tunayoweza kujifunza kwa sasa kuhusu hekima. Ninawaahidi kwamba baraka za Bwana zitawajia pale mtakapotafuta hekima, hekima ya Mungu. Anapenda sana kutoa hekima Zake kwetu. Na kama tutakuwa watiifu na wakuomba na kuhitaji, itakuja.