Ushawishi wa Kiroho wa Wanawake
Mwandishi anaishi Utah, Marekani.
Je, tunajua uwezo wa nguvu zetu za kiroho?
Wanawake wengi, wanyenyekevu katika Kanisa hutoa huduma ya kujitolea bila kutambua athari ya kina ambayo hutokana na maisha yao kuwa—kama mifano ya huduma ya kidunia, lakini pia kama urithi wa nguvu za kiroho. Mmoja wa wanawake hao ni bibi yangu, Cherie Petersen. Amehudumu kwa uaminifu katika miito ya kimya kimya katika maisha yake yote. Ukimuuliza, angedai kwamba hana vipaji vingi vya kutoa kwa dunia. Hata hivyo, nilivyoanza kujifunza kuhusu maisha yake, niligundua kiwango ambacho nguvu yake ya kiroho ilivyoathiri maisha yangu.
Wazazi wa Cherie waliacha kuhudhuria kanisa na wakatalikiana wakati alipokuwa bado mdogo sana, hivyo basi alilelewa na mama, Florence, ambaye alikuwa daima anafanya kazi. Florence alikuwa hata ametelekezwa zaidi akiwa mtoto, kwani alilelewa katika shule za bweni wakati mama yake, Georgia, akiishi maisha ya kilimwengu. Licha ya changamoto katika malezi yake, Cherie alibakia akijishughulisha na injili, kwa uaminifu akihudhuria kanisa na marafiki wa bibi yake mkongwe Elizabeth au na marafiki wengine. Aliona katika familia zao kile alichokitaka kwa familia yake mwenyewe. Hakujua hasa jinsi familia inavyopaswa kuwa, lakini alijua jinsi iisivyopaswa kuwa, na alidhamiria kuwa familia yake ya siku za usoni iwe tofauti.
Mumewe Cherie—babu yangu Dell—wakati mmoja aliniambia, “Ili kuwa na ushuhuda lazima uutake. Cherie daima aliutaka ushuhuda.” Ingawa miaka yao ya awali ya ndoa ilijawa na shida, walidhamiria kubaki imara kama familia. Walikuwa hawahudhurii kanisa kila mara katika mwaka wa kwanza wa ndoa yao kwa sababu ya ratiba ya kazi ya Dell, lakini wito kuhudumu kwa Watoto ulisababisha Cherie kuanza kuhudhuria, na Dell punde alijiunga naye kanisani kama mshauri wa akidi ya washemasi. Wote wamehudhuria kanisani na kuwa imara katika Kanisa tangu wakati huo. Kutaka kwa Cherie kuhudumu na uamuzi wa kujenga familia imara kulimsaidia mamangu kuwa mwanamke mwenye nguvu, na mfano wa mamangu umesaidia kuongoza maisha yangu, hasa ninapoanzisha familia yangu mwenyewe sasa.
Kama wanawake tunaweza kuwa na ushawishi wa kina wa kiroho katika maisha ya wale wanaotuzunguka. Hakika, Joseph Smith alifundisha kwamba jukumu letu “siyo tu kuwasaidia maskini, lakini kuokoa”.1 Yesu Kristo ametoa wito kwa wanawake wa Kanisa Lake kuwa wafuasi wake na kuwa na nguvu kiroho. Nguvu na ushawishi wetu wa kiroho ni muhimu katika maendeleo ya kazi ya wokovu, na tunapaswa tutafute fursa za kuwaimarisha kiroho wanaotuzunguka. Tunapofanya hivyo, ushawishi wa imani na wema wetu utadumu zaidi kupita kile tunachoweza kuona.
Kuitwa Kuwa Wafuasi
Mzee James E. Talmage (1862–1933) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili aliandika, “shujaa mkuu duniani wa mwanamke na umama ni Yesu Kristo”.2 Fikiria, kwa mfano, juu ya kile alichowafundisha wafuasi Wake wawili wa kike katika Agano Jipya, kina dada Mariamu na Martha. Kitabu Daughters in My Kingdom kinaelezea: “Luka 10 kina taarifa ya Martha akifungua nyumba yake kwa Yesu. Alimhudumia Bwana kwa kutekeleza mahitaji yake ya kimwili, na Mariamu alikaa miguuni pa Mwalimu na kupokea mafundisho yake.
Katika umri ambapo wanawake walitarajiwa kwa ujumla kutoa huduma ya kimwili tu, Mwokozi alimfundisha Martha na Mariamu kuwa wanawake pia wangeweza kushiriki kiroho katika kazi Yake. Aliwaalika wawe wanafunzi Wake na kushiriki wokovu, sehemu ile nzuri’ ambayo kamwe haitachukuliwa kutoka kwao.”3
Kama Martha, wakati mwingine sisi hukosea kufikiri kwamba jukumu la msingi la wanawake ni kutoa huduma ya kimwili, kama vile kutoa milo, kushona, na kuwasafishia wengine. Huduma hii ni muhimu na bora kabisa; Hata hivyo, hata zaidi ya anavyo wahitaji kina dada ambao wanaweza kushona na kupika, Bwana anawahitaji wanawake walio na nguvu za kiroho ambao imani, wema na hisani vinang’aa katika maisha yao. Anajua kwamba sote tuna mengi ya kutoa. Yesu Kristo anamwita kila mmoja wetu kukuza nguvu zetu za kiroho na uwezo wa kupokea na kutenda juu ya ufunuo wa kusaidia kusogeza kazi Yake mbele. Linda K. Burton, Rais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, alisema kwa akina dada, “Mmetumwa duniani katika kipindi hiki cha nyakati kwa sababu ya asili yetu na kile mlichoandaliwa kufanya! Bila kujali nini Shetani angejaribu kutushawishi kufikiri kuhusu asili yetu, utambulisho wetu wa kweli ni ule wa mfuasi wa Yesu Kristo!”4
Bwana anatujua na hali zetu, na Anayo kazi kwa kila mmoja wetu kufanya katika dunia hii. Hakuna dada anayejua kidogo sana au aliye na vipaji vichache kuwa nguvu ya kiroho kwa ajili ya wema na kuwaleta wengine kwa Kristo. Kwa uwezo huu wa kiungu tuna wajibu wa kuwa viongozi wa kiroho katika nyumba zetu na jumuiya zetu. Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitangaza, “Kila dada katika Kanisa ambaye amefanya maagano na Bwana ana jukumu takatifu la kusaidia kuokoa nafsi, na kuongoza wanawake wa ulimwengu, kuimarisha nyumba za Sayuni, na kujenga ufalme wa Mungu.”5
Si lazima tuwe katika nafasi za juu au kufanya mambo yasiyo ya kawaida ili kusaidia wale wanaotuzunguka wafanye maamuzi ambayo yatawaelekeza kuwa karibu na Yesu Kristo—ambao ni wajibu wetu muhimu sana. Yote mambo madogo na makubwa tunayofanya katika maisha ya mtu mmoja au wawilii, hata ndani tu ya familia zetu wenyewe, yanaweza kuwa na athari kubwa.
Wanawake katika Kazi ya Wokovu
Wimbo tunaoupenda unaeleza, “Kazi za malaika wamepewa wanawake; Na hii ni zawadi ambayo, kama akina dada, tunaidai.”6 Tuna mengi ya kutoa katika maisha ya wale tunaowapenda. Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili amesimulia hadithi ya jinsi nguvu ya kiroho ya wanawake wawili ilivyoathiri maisha yake:
“Nilipokuwa mtoto mdogo, baba yangu hakuwa muumini wa Kanisa na mama yangu alikuwa hahudhurii kanisani. Miezi kadhaa baada ya sikukuu yangu ya nane ya kuzaliwa, Bibi Whittle alikuja kutoka upande wa pili wa nchi kututembelea. Bibi alikuwa na wasiwasi kwamba, mimi na kaka yangu tulikuwa hatujabatizwa. Sijui aliwaambia nini wazazi wangu kuhusu haya, lakini najua kwamba asubuhi moja alimchukua ndugu yangu pamoja na mimi kwenye bustani na kushirikiana nasi hisia zake kuhusu umuhimu wa kubatizwa na kuhudhuria mikutano ya Kanisa kila mara. Sikumbuki yale yote aliyoyasema, lakini maneno yake yalichochea kitu katika moyo wangu, na punde baadaye ndugu yangu pamoja na mimi tulibatizwa. …
Bibi alitumia kiasi sahihi cha ujasiri na heshima ili kumsaidia baba yetu kutambua umuhimu wake kwa kutuendesha kwenda kanisani kwa ajili ya mikutano yetu. Katika kila njia sahihi, alitusaidia sisi kuona umuhimu wa injili katika maisha yetu”.7
Chanzo cha pili cha nguvu za kiroho alikuwa mke wa Mzee Scott, Jeanene. Walipokuwa katika matembezi ya kirafiki walianza kuzungumza kuhusu siku zijazo. Jeanene, ambaye alikuwa amelelewa katika nyumba imara ya kimisionari, alionyesha hamu yake kuolewa katika hekalu na mmisionari aliyerejea nyumbani. Mzee Scott, ambaye hakuwa amefikiria kuhusu kuhudumu misheni kabla, aliguswa kwa nguvu sana. “Nilienda nyumbani, na sikuweza kufikiria kuhusu kitu chochote kingine. Nilikuwa macho usiku mzima. Baada ya sala nyingi nilifanya uamuzi wa kukutana na Askofu wangu na kuanza maombi yangu ya umisionari”.8 Ingawa Jeanene alimpa uongozi na ushawishi aliohitaji, Mzee Scott alisema, “Jeanene kamwe hakuniomba nihudumu misheni kwa ajili yake. Alinipenda vya kutosha kushirikiana nami ushuhuda wake na kisha alinipa fursa ya kuelekeza mwelekeo wa maisha yangu menyewe. Sisi sote tulihudumu misheni na baadaye tuliunganishwa katika hekalu. Ujasiri na msimamo wa Jeanene kwa imani yake ulifanya tofauti yote katika maisha yetu kwa pamoja. Nina uhakika hatungepata furaha tunayoifurahia bila imani yake imara katika kanuni ya kumtumikia Bwana kwanza. Yeye ni mfano wa ajabu, mfano wema!”9
Ilikuwa ushawishi wa kiroho wa hawa malaika wanawake katika maisha yake kwamba walisaidia tu kijana mmoja—Mzee Scott—kufanya baadhi ya maamuzi muhimu katika maisha yake: kubatizwa, kutumikia misheni, na kuoa katika hekalu.
Tunaweza kuwasaidia wengine kufanya maamuzi mazuri kutokana na mfano wetu, matendo, maneno, na wema wetu binafsi. Dada Carole M. Stephens, mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, anatangaza, “Sisi ni mabinti wa agano katika ufalme wa Bwana, na tuna fursa ya kuwa vyombo katika mikono yake. Tunashiriki katika kazi ya wokovu ya kila siku kwa njia ndogo na zilizo rahisi—“kulinda, kuimarisha na kufundishana sisi kwa sisi.”10 Tunapotegemea Roho na kusonga mbele katika juhudi za dhati na nyenyekevu kuwasaidia wale walio karibu nasi kuja karibu na Kristo, tutaongozwa katika kile tunachoweza kufanya na kupatiwa nguvu ya kukifanya, na tutasikia furaha ya kuwaleta watoto wa Bwana Kwake.
Kuwa Ushawishi wa Kiroho
Kujua jukumu letu, tunaweza kuuliza kama wanafunzi wa zamani, “Tutendeje” (Matendo 2:37) ili kuwa na ushawishi wa kiroho? Katika mkutano mkuu wa hivi karibuni, Dada Burton aliwaalika akina dada kufikiria “baadhi ya misaada ya kiroho inayoweza kuwa ‘msaada unahitajika’ ishara zinazohusiana na kazi ya wokovu:
-
Msaada unahitajika: wazazi kulea watoto wao katika mwanga na ukweli
-
Msaada unahitajika: binti … , akina dada. shangazi … , binamu, mababu, na marafiki wa kweli kutumika kama washauri na kutoa mikono ya usaidizi kwenye njia ya agano
-
Msaada unahitajika: wale wanaosikiliza ushawishi wa Roho Mtakatifu na kuyatendea kazi mawazo wanayopokea
-
Msaada unahitajika: wale wanaoishi injili kila siku kwa njia zilizo ndogo na rahisi
-
Msaada unahitajika: wafanyikazi wa historia ya familia na hekalu ili kuunganisha familia milele
-
Msaada unahitajika: wamisionari na waumini kueneza habari njema—“injili ya Yesu Kristo”
-
Msaada unahitajika: waokozi kuwatafuta wale ambao wamepotea njia yao
-
Msaada unahitajika: wanaoshika maagano kusimama imara kwa ajili ya ukweli na haki
-
Msaada unahitajika: wafuasi wa kweli wa Bwana Yesu Kristo”.11
Haya si mambo mapya, lakini wakati tunapotafuta fursa ya kushiriki katika kazi ya wokovu, tutaboresha uwezo wetu wa kuwasaidia wale wanaotuzungukai. Mzee Ballard alisema, “Hakuna kitu katika dunia cha kibinafsi, kama kuwalea, au kama kubadilisha maisha kama ushawishi wa mwanamke mwema.”12 Tunapokuza nguvu zetu za kiroho kwa njia ya sala binafsi na mafunzo ya maandiko, utii imara, na kushika maagano yetu kwa uaminifu, tutakuwa ushawishi huo.
Zaidi ya Kile Tunachoweza Kuona
Rais Brigham Young (1801–1877) alisema, “Je, unaweza kuona kiasi cha wema ambao kina mama na mabinti katika Israeli wanaoweza kufanya? Hapana, haiwezekani. Na wema watakaofanya utawafuata milele.”13
Maamuzi ya haki ya bibi yangu yameathiri vizazi vya familia yake kupita kile ambacho yeye kama msichana angeweza kukiona. Hata hivyo, ushawishi wa kiroho wa wanawake katika familia yangu unapanuka hata mbali zaidi kurudi nyuma. Cherie alipata sehemu kubwa ya nguvu zake mwenyewe za kiroho kwa kumtazama bibi yake (bibi yangu wa kizazi cha tatu nyuma) Elizabeth. Mfano wa Elizabeth wa imani na ushuhuda ulifika kupita vizazi viwili vya kutohudhuria kanisa ili kumsaidia kitukuu wake Cherie kubadili mwelekeo wa familia zilizovunjika na kurudi katika Kanisa.
Tunapokuwa nguvu ya kiroho kwa wale wanaotuzunguka, ushawishi wetu utafika mbali zaidi ya kile tunachoweza kukiona. Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) alisema, “Tunawaomba wanawake wa Kanisa wasimame pamoja kwa ajili ya wema. Ni lazima waanze katika nyumba zao wenyewe. Wanaweza kufundisha katika madarasa yao. Wanaweza kutoa sauti katika jumuiya zao. …
“Ninaona hii kama tumaini moja linalong’aa katika dunia inayoelekea katika kujiangamiza yenyewe.”14
Tunapotimiza amri hii, kazi ya Bwana itasonga mbele kote katika dunia inayotuzunguka na, muhimu zaidi, katika familia zetu na maisha ya wale tunaowapenda.