Kwa Watoto Wadogo Ninajua Kwamba Yesu Ananipenda Na Jane McBride Choate Imetokana na tukio halisi Mwandishi anaishi katika Colorado, Marekani. Laney alikuwa anajaribu sana kuwa na staha kanisani. Lakini alikuwa amechoka, miguu yake ilianza kulegea. Baada ya sakramenti kuisha, Laney alifungua kitabu chake juu ya Yesu. Alipata picha ya Yesu na watoto wadogo. Ilimfanya kusikia amani na furaha ndani yake. Baada ya mkutano wa sakramenti kumalizika, Laney alimwuliza Mama, “Kwa nini ni rahisi kuwa na staha ninapotazama kitabu changu juu ya Yesu?” “Ninafikiri ni kwa sababu kinakukumbusha jinsi Yesu anavyokupenda,” Mama akasema. Laney alikubali kwa kichwa. “Unafikiri Yesu anajua kuwa ninampenda pia?” akauliza. Mama akamkumbatia Laney. “Ndiyo nina hakika anajua.” I Know That My Savior Loves Me Tami Jeppson Creamer and Derena Bell