Ujumbe wa Urais wa Kwanza
Rais Monson Ahimiza Ujasiri
Hata saa moja haipiti, Rais Thomas S. Monson ameelezea, kwamba tunahimizwa kufanya chaguzi za aina moja ama nyingine.
Ili kufanya chaguzi za hekima, alishauri, tunahitaji ujasiri—“ujasiri wa kusema hapana, ujasiri wa kusema ndio. Maamuzi huamua hatima.”1
Katika dondoo zifuatazo, Rais Monson anawakumbusha Watakatifu wa Siku za Mwisho kwamba wanahitaji ujasiri kusimama kwa ajili ya ukweli na haki, ili kutetea kile wanachoamini, na kukabiliana na ulimwengu ambao unakataa maadili na kanuni za milele.
“Wito wa ujasiri huja kila mara kwa kila mmoja wetu, alisema. Imekuwa hivyo, na hivyo ndivyo itakavyokuwa milele.”2
Ujasiri Huleta Idhini ya Mungu
Sote tutakabiliwa na hofu, tutafanyiwa kejeli, na kukutana na upinzani. Sisi,—sisi sote—tuwe na ujasiri wa kwenda kinyume na yanayokubalika, ujasiri wa kusimama kwa ajili ya kanuni. Ujasiri, kuto kubali maovu, huleta tabasamu ya idhini ya Mungu. Ujasiri huwa adili hai na ya kuvutia unapochukuliwa si tu kama kutaka kufa kiume lakini pia kama uamuzi wa kuishi vyema. Tunaposonga mbele, tukijitahidi kuishi kama tunavyopaswa, hakika tutapata usaidizi kutoka kwa Bwana na tunaweza kupata faraja katika maneno Yake.”3
Shinda kwa Ujasiri
“Nini maana ya kustahimili? Ninapenda maana hii: kushinda kwa ujasiri. Ujasiri unaweza kuhitajika kwako katika kuamini; utahitajika wakati mwingine unapotii. Kwa hakika utahitajika zaidi kadiri unavyo stahimili hadi siku ile utakapoondoka katika maisha haya ya duniani.”4
Kuwa na Ujasiri wa Kusimama kwa ajili ya Ukweli
“[Na] uwe na ujasiri wa kusimama imara kwa ajili ya ukweli na haki. Kwa sababu mwenendo katika jamii ya leo uko mbali na maadili na kanuni ambazo Bwana ametupa, bila shaka utaitwa utetee yale ambayo unayaamini. Isipokuwa mizizi ya ushuhuda wako imepandwa imara, itakuwa vigumu kwako wewe kustahimili kejeli ya wale wanaoijaribu imani yako. Ukiwa umepandwa imara, ushuhuda wako wa injili, wa Mwokozi, na wa Baba yetu wa Mbinguni utashawishi yote unayoyafanya katika maisha yako.”5
Tunahitaji Ujasiri wa Kiroho na wa Maadili
“Ujumbe unao onyeshwa kwenye televisheni, katika sinema, na katika vyombo vingine vya habari [leo] mara nyingi sana uko kinyume kabisa na ule ambao tunataka watoto wetu waupokee na waushikilie kwa dhati. Ni wajibu wetu, si tu kuwafundisha kuwa imara katika mafundisho na katika roho lakini pia kuwasaidia kukaa hivyo, bila kujali nguvu za nje wanazoweza kupambana nazo. Hii itahitaji muda na juhudi nyingi kwa upande wetu—na ili kuwasaidia wengine, sisi wenyewe tunahitaji ujasiri wa kiroho na kimaadili ili kustahimili mabaya tunayoona kila upande.”6
Tuweze Daima Kuwa Wajasiri
“Tunapoendelea kuishi siku baada ya siku, ni dhahiri kabisa kwamba imani yetu itapata changamoto. Tunaweza saa zingine kujikuta tumezungukwa na watu wengine na bado tukiwa tumesimama katika wale wachache ama hata kusimama pekee yetu kuhusu kile ambacho kinakubalika na kile ambacho hakikubaliki.
Na tuweze daima kuwa wajasiri na tuliojitayarisha kusimama kwa ajili ya yale tunayoamini, na ikiwa lazima tusimame pekee yetu katika mchakato huu, tuweze kufanya hivyo kwa ujasiri, tukiwa tumeimarishwa na ufahamu kwamba kwa ukweli kamwe hatuko pekee yetu tunaposimama na Baba yetu aliye Mbinguni.”7