2015
Nabii Aliyehai
Aprili 2015


“Nabii aliye hai ni muhimu zaidi kwetu kuliko yule aliye kufa. …

Ufunuo wa Mungu kwa Adam haukumwelezea Nuhu jinsi ya kujenga Safina. Nuhu alihitaji ufunuo wake mwenyewe. Kwa hiyo, nabii aliye muhimu sana, kadiri mimi na wewe inavyotuhusu , ni yule anayeishi katika siku na zama zetu ambaye Bwana kwa sasa anamfunulia mapenzi yake kwa ajili yetu. Kwa hiyo, somo muhimu sana tunaloweza kufanya ni maneno yoyote ya nabii ambayo yanapatikana kwenye majarida ya Kanisa ya kila mwezi. Mwongozo wetu kwa kila miezi sita unapatikana kwenye mafundisho ya mkutano mkuu, ambayo yanachapishwa kwenye [Liahona] jarida.

Kuweni waangalifu kwa wale watakao wadharau manabii waliokufa dhidi ya manabii walio hai, kwani manabii walio hai mara zote huchukua nafasi ya kwanza.

Na Rais Ezra Taft Benson (1899–1994), “Misingi na kanuni Kumi na Nne katika Kumfuata Nabii” (Brigham Young University devotional, Feb. 26 1980), 2, speeches.byu.edu.