2015
Kundi Moja na Mchungaji Mmoja
Aprili 2015


Kundi Moja na Mchungaji Mmoja

Boma la kundi la kondoo hutufundisha kuhusu ulinzi wa Mwokozi kwa watu Wake.

Zizi la Kondoo la Kale

Gogo (kizuizi)

Mchungaji

Kuta za mawe

Mlango

Kondoo

Kombeo

Fimbo

Ni nini: Zizi la kawaida, Boma la kuta.

Dhamira: Kulinda kundi la kondoo kutokana na wauaji, wezi hasa usiku

Vifaa na ujenzi: Mawe, kwa kawaida, na vichaka vyenye miiba mara kwa mara huwekwa juu ya kuta, Matawi makubwa yenye miiba pia yalitumika mara kwa mara kutengeneza ua la zizi la muda mfupi. Mapango wakati mwingine yalitumika kama zizi, na jiwe la wastani dogo au vizuizi vya miiba vikiwekwa mbele yake.

Kile Tunachoweza Kujifunza

Zizi za kondoo ni:

Pale ambapo kondoo hukusanyika. Kama waumini wa Kanisa, tunashiriki mfungo wa umoja kupitia kwa imani yetu na maagano yetu, na pia kwa kihalisi kukusanyika pamoja. Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza, amefundisha: “Furaha ya umoja [Baba wa Mbinguni] anataka sana kutupa sisi, sisi si pweke. Ni lazima tuitafute na kustahili pamoja na wengine. Si ajabu basi kuwa Mungu anatuhimiza kukusanyika pamoja ili Yeye aweze kutubariki. Anataka tukusanyike katika familia. Alianzisha madarasa, kata, na matawi na kutuamuru kukutana kila mara. Tunaweza kuomba na kufanyia kazi umoja huo utakaotuletea furaha na kuongeza uwezo wetu wa kuhudumu” (“Our Hearts Knit as One,” Liahona, Nov. 2008, 69).

Mahali pa usalama na pumziko. Katika Yesu Kristo “tunapata raha nafsini [mwetu]” (Mathayo 11:29). Kanisa Lake ni “ngome, na … kimbilio” (M&M 115:6). Na kama vile Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyofundisha, “Tunapata usalama na ulinzi kwetu wenyewe … katika kuheshimu maagano tuliyofanya na kuishi kulingana na matendo ya kawaida ya utiifu yanayohitajika kwa wafuasi wa Kristo” (“These Things I Know,” Liahona, May 2013, 7).

Kulindwa na Mchungaji. Yesu Kristo ni Mchungaji Mwema anayetuokoa. Aliteseka na kufa ili tuweze kushinda dhambi na kifo na kurejea kwaBaba yetu wa Mbinguni Tunapokuja kwa Kristo na kuwa watiifu kwa amri Zake, Anatubariki, Anatuongoza, na kutulinda sisi binafsi na kama watu wake wa agano.