2015
Roho Alininong’oneza
Aprili 2015


Roho Alininong’onezea

Christina Albrecht Earhart, Washington, USA

drawing of boys running

Vielelezo na Bradley H. Clark

“Enyi, jamaa! Rudini!” sauti yenye majonzi ikaita.

Nikageuka na kuwaona wavulana wawili wenye umri wa miaka karibu mitano na saba wakikimbia kwenye sehemu ya maegesho ya magari machozi yakiwatiririka chini ya nyuso zao. Muuzaji alikuwa na wasiwasi wakati anawaita.

Nilipogeuka upande wa gari langu, Roho alininong’oneza, “Unaweza kuwa msaada hapa.” Mnong’ono ulikuwa wa kimya lakini dhahili kwamba muda mfupi baadaye nilikuwa nikikimbia kwenye maegesho ya magari kuelekea kwa wale wavulana.

Nilimkuta yule mkubwa amesimama karibu na minivani ya kahawia. Nilimsogelea na kupiga magoti pembeni yake.

“Helo. Jina langu ni Christina. Je uko salama?”

Baada ya maneno yangu, alilia zaidi na kuuficha uso wake katika mikono yake. Muuzaji na mvulana mwingine walijumuika nasi.

“Nafikiri wanaongea Kifaransa pekee,” muuzaji aliniambia. “Ndiyo kwanza Tuliwaona wakikimbia kupitia dukani, wamepotea.”

Nikarudia utambulisho kwa wale watoto kwa Kifaransa. Kifaransa kilikuwa ndiyo lugha yangu ya kwanza, lakini nimekuwa siitumii toka nilipo asiliwa na familia inayoongea-Kiingereza nikiwa mtoto mdogo. Kwa kawaida, Kifaransa changu si-kizuri. Kwa wakati huo, hata hivyo, hakikuwa sio stadi wala rasmi. Maneno yalikuwa wazi katika fikra zangu na sauti yangu wakati nawafariji wale wavulana.

Katikati ya kilio cha kwikwi,kijana mkubwa alieleza kwa mbubujiko wa haraka wa maneno kwamba yeye na ndugu yake hawakuweza kuwaona wazazi wao mahali popote katika duka na ilibidi wakimbie nje ya duka kuwatafuta. Nilipokuwa nasikiliza,niliweza kwa mashaka kutambua kwa jinsi ya kushangaza ilikuwa kwamba sikuwa tu naongea kwa uhuru kifaransa lakini pia bila shida kuelewa na kufariji watoto wawili waliotishika.

“Wamepotezana na wazazi wao na wanataka kuwasubiri hapa kwenye gari lao,” nikamwambia muuzaji. Mvulana mdogo alinitajia majina ya wazazi wake, ambayo nilimpa muuzaji ili awaite kwa kipaza sauti. Dakika chache baadaye mvulana akamwona baba yake akitoka nje ya duka na kukimbia ili kumlaki.

Nilipokuwa namfuata yule mvulana kwa baba yake, nikagumdua kwamba nilishindwa hata kusema kwaheri kwa Kifaransa. Nilijaribu kuongea chochote ambacho wale wavulana wangenielewa, lakini nilishindwa kusema chochote zaidi ya maneno mchanganyiko. Mwishowe, nikarudi kwenye Kiingereza, nikimwambia yule mvulana, “Kwaheri. Ilikuwa vizuri kukutana nawe.”

Nilipowaacha wale wavulana na wazazi wao, nilijawa na shukrani. Baba wa Mbinguni alifanyakazi kupitia mimi ili kuwafariji watoto Wake wawili. Nilikuwa na unyenyekevu kwamba Bwana alikuwa ameongeza uwezo wangu mdogo ili kutimiza nia Yake. Nilikuwa na shukurani kushuhudia nini kinaweza kutokea tunapojitoa wenyewe Kwake pale tunapoitwa, hata sehemu isiyowezekana.