Nyumba Zetu, Familia Zetu
Jioni ya Familia Nyumbani—Mnaweza Kuifanya!
Haidhuru familia yako ikoje, jioni ya familia nyumbani inaweza kuwabariki na kuwaimarisha.
Baba anafika nyumbani akiwa amechoka baada ya siku ndefu kazini na huwakuta wengine katika familia yake wakihangaika na hisia hizo za uchovu. Ni Jumatatu usiku, na kufanya jioni ya familia nyumbani kunaonekana kutowezekana. Baada ya kusema sala kwa ajili ya msaada, baba na mama wanaamua kufanya mambo kwa urahisi. Wanaita familia yao pamoja, wanaimba wimbo, na kusali pamoja. Wanampa kila mwana familia mshumaa mdogo kuwasha huku wakielezea kuhusu jambo lililowavutia hivi karibuni. Katika chumba kilicho na giza, mwanga wa mishumaa unawakilisha uvuvio na unalenga usikivu wa watoto. Shuhuda zinapokuwa zikitolewa, hisia ya amani tamu na upendo zinaingia nyumbani. Familia inakamilisha usiku kwa shukurani kwamba wamefanya jioni ya familia.
Je, unajua kwamba jioni ya familia nyumbani imekuwa mpango wa Kanisa kwa miaka 100? Mnamo Aprili 1915, Urais wa Kwanza uliwaagiza waumini watenge usiku mmoja kila wiki kwa ajili ya sala ya familia, muziki, kujifunz injili, hadithi, na shughuli nyinginezo. (Ona ukurasa 80 kwa dondoo kutoka barua ya Urais wa Kwanza.) Manabii wanaendelea kutukumbusha umuhimu wa jioni ya familia nyumbani. “Hatuwezi kumudu kupuuza mpango huu wa maongozi kutoka mbinguni, Rais Thomas S. Monson alisema. Unaweza kuleta ukuaji wa kiroho kwa kila mwana familia, kumsaidia kuhimili vishawishi ambavyo vipi kila mahali.”1
Hapa ni baadhi ya fikra za kukumbuka unapoifanya jioni ya familia nyumbani kuwa sehemu yako ya wiki:
Hii inahusika na mimi. “Jioni ya familia nyumbani ni kwa kila mtu,” alisema Mzee L. Tom Perry wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.2 “Sisi sote—tuliooa ama bado, tulio na watoto au la—tunaweza kutoa muda kuimarisha familia na kujifunza injili”.
Naweza kupata muda. Kanisa linaweka mfano kwa kuacha Jumatatu usiku kuwa bila shughuli za Kanisa. Unaweza kumwoonyesha Bwana na familia yako kuwa uko tayari kutenga muda kwa kile kilicho cha muhimu zaidi.
Naweza kupata kile kinachowezekana kwa familia yangu. Kama familia yako imetengwa kijiografia, jaribu jioni ya familia kupitia intaneti na zungumza na wanafamilia kupitia intaneti au kwenye simu. Je, kuna mtu anayelazimika kufanya kazi hadi usiku sana? Fanya jioni ya familia nyumbani kwenye bustani” iliyo karibu na kazini wakati wa mapumziko. Baba aliyekuwa ameachwa na mke alifanya jioni ya familia kupitia barua kila Jumatatu, akiwaandikia watoto wake ambao waliishi mbali.3 Fanya vikwazo viwe kichocheo kwa ajili ya ubunifu zaidi.
Naweza kuanza wiki hii. Jioni ya familia nyumbani inaweza kupangwa kulingana na mahitaji na hali ya nyumba yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo kwa ujumla:
-
Anza na umalize kwa sala.
-
Tumia muziki, ikiwa ni pamoja na nyimbo za kanisa na nyimbo za Watoto.
-
Jifunze kutoka katika maandiko na manabii wa kisasa.
-
Jumuisha aina mbali mbali ya michezo, miradi ya huduma, na shughuli zilizojengeka katika misingi ya injili wiki baada ya wiki.
-
Pateni Burudani! Cheza mchezo au tayarisha viburudisho.
-
Fanyeni mfululizo. Kama huwezi kufanya Jumatatu, tafuteni siku nyingine ambayo inawezekana.
Nataka baraka. Manabii wameahidi kwamba endapo tukishiriki katika jioni ya familia nyumbani, baraka kubwa itatokea: Upendo na utiifu nyumbani utaongezeka. Imani itakua katika mioyo ya vijana. Familia “itapata nguvu ya kupambana na athari mbaya na majaribu yanayo wazingira” wao.4
Huku jioni zako za familia nyumbani inawezekana zisiwe matukio safi kila wakati, familia yako itaimarishwa na kubarikiwa kwa sababu ya juhudi zako. “Kila jioni ya familia nyumbani ni alama kwenye turubai la roho zetu”, Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha. “Hakuna tukio moja linaloweza kuonekana kuwa la kuvutia sana au kukumbukwa. Lakini kama vile tu alama za rangi zinavyo kamilishana vyema na kuzalisha picha inayovutia, hivyo pia msimamo wetu wa kufanya mambo yanayoonekana kuwa madogo kunavyoweza kusababisha matokeo muhimu ya kiroho.”5