2015
Nina Haja Nawe Kila Saa
Aprili 2015


“Nina Haja Nawe Kila Saa”

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

Wakati tulipokuwa hatujui nini zaidi tunachoweza kufundisha, mwenzangu alipendekeza tuimbe wimbo huu.

drawing of family with missionaries

Jumapili moja mchana katika misheni yangu huko Balsan, Korea, mmisionari mwenzangu na mimi tulikuwa tunasema kwaheri kwa waumini baada ya kanisa na tulikuwa karibu kuondoka kwenda kufundisha wakati kiongozi wa misheni wa kata alipotutambulisha kwa kijana mwenye umri wa miaka 12, Kong Sung-Gyun. Alikuwa amehudhuria kanisa siku hiyo na alitaka kujifunza zaidi kuhusu injili.

Bila shaka tulikuwa na furaha kuhusu matarajio ya kumfundisha, lakini pia nilikuwa na woga kuhusu kufundisha kijana mdogo vile. Tuliamua kuhakikisha tunapata na ruhusa ya wazazi wake, hivyo basi nilipiga simu nyumbani kwa Kong Sung-Gyun na kuongea kwa kifupi na mama yake, Pak Mi-Jung. Nilishangazwa wakati aliposema alifurahi mwanawe alikuwa anafikiria kuhudhuria kanisa na kwamba angefurahia afundishwe nasi.

Wachunguzi Wasiotarajiwa

Jioni ya pili tulifika nyumbani kwa kijana yule, tayari kufundisha. Tulishangaa kujua kwamba Pak Mi-Jung pia alitaka tumfundishe na binti yake, Kong Su-Jin. Na kwa kuwa tulikuwa wageni katika nyumba yake, Pak Mi-Jung alitaka kukaa katika mafundisho. Bila shaka tulikuwa na furaha kufundisha wengi wa waliotaka kusikiliza.

Baada ya kutupa vinywaji, tuliketi pamoja na kuanza kuzungumza. Badala ya kuanza moja kwa moja na somo, Pak Mi-Jung alitaka kutujua vyema zaidi na kutuelezea kuhusu hali ya familia yake. Alituambia kuhusu majaribu ya hivi karibuni na matatizo waliyokuwa wamepitia, ikiwa ni pamoja vita vya mwanawe vya hivi karibuni na saratani. Alikuwa amepitia mafanikio ya matibabu ya mionzi, na saratani ilikuwa kwa sasa katika hali ya kuondoka, lakini madaktari waliwaonya ingerudi wakati wowote. Huu ulikuwa mzigo mkubwa kwa familia. Walikuwa famila ya kipato cha kawaida, na baba alilazimika kufanya kazi kwa nguvu sana ili kuweza kuwa na nyumba na chakula.

Nilishangazwa na kuhuzunishwa na majaribu katika maisha yao. Maisha hayakuwa rahisi kwao, lakini ukaribu ndani ya familia ulikuwa dhahiri zaidi kuliko nilivyokuwa nimeona katika familia nyingine yo yote ambayo nilikuwa nimekutana nayo Korea, ambayo inasema mengi katika jamii ya kifamilia za Korea. Sisi tuliondoka nyumbani kwao jioni hiyo baada ya kujuana vyema na familia hii maalum na baada ya kuwafundisha ujumbe wa injili.

Mwenzi wangu na mimi tulirudi kufundisha mara kadhaa zaidi wiki hiyo, kila wakati tukipata ukujufu na ukarimu sawa na ule tuliopata katika matambezi yetu ya kwanza. Wakati mada ya ubatizo ilipokuja, watoto wawili walikuwa na hamu sana kujiunga na Kanisa. Hata hivyo, mama yao hakushiriki katika msisimko wao. Ingawa mafundisho yetu yalimwingia na alitumaini kuwa ni ya kweli, yeye hakuona kama angeweza kufanya na kuwa na aina ya msimamo ambao Kanisa linataka unapojiunga nalo. Yeye pia hakuona kwamba ingekuwa sahihi kwake yeye kubatizwa bila mumewe, ambaye tulikuwa bado kukutana naye. Hata hivyo, yeye alikuwa na nia ya kuendelea kukutana na sisi na pia alitaka kujiunga na watoto wake katika kuhudhuria kanisa.

Karibu na mwisho wa wiki ya pili, tulipokuwa tukiendelea kufundisha katika nyumba yake, tulikutana na mume wake, Kong Kuk-Won—mnyenyekevu, mwenye subira, na mtu mkarimu. Yeye alijiunga na sisi kwa majadiliano machache ya kumalizia na papo hapo aliamini kila kitu tulichowafundisha, ikiwa ni pamoja na mafundisho ambayo mara nyingi wengine waliyaona vigumu kama vile zaka na Neno la Hekima. Pamoja na hali zao kuwa duni ki fedha, walianza kulipa zaka. Kikwazo pekee kwa baba kilikuwa kufanya kazi kila siku ya Jumapili. Yeye alifanya kazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Seoul kila Jumapili, hivyo hakuweza kuhudhuria kanisa na wengine wa familia yake. Pamoja na ratiba ya kazi yake, yeye na mke wake walipanga kuhudhuria ubatizo ya watoto wao Jumapili iliyofuata.

Kufuatia ubatizo wa watoto wao, tuliendelea kukutana mara kwa mara katika nyumba ya familia. Tulikuwa na jioni ya familia nyumbani, tulishiriki maandiko na matukio ya kuvutia, na kuwatambulisha kwa waumini wa kata. Hata hivyo, licha ya uzoefu wa kuendelea wa injili, wazazi hawakuwa karibu kubatizwa.

Wakati huo huo mwenzi wangu mmisionari alihamishwa, na mwenzi mpya alikuwa mmisionari aliyetoka punde kutoka kituo cha mafunzo cha umisionari. Alijawa na imani, nguvu, na hamu, na kwa kweli nilikuwa na wakati mgumu kuafikiana naye. Baada ya kukutana na Kong Kuk-Won na Pak Mi-Jung mara chache, mwenzi wangu alinijia na kuuliza kama mwenzangu wa awali pamoja nami tulikuwa tumefunga pamoja nao. Hatukuwa tumefunga nao Kwa kweli, wazo hilo halikuwa limewahi kunijia. Hivyo tulikutana na familia na kupendekeza kufunga. Nilishtuka kugundua kuwa walikuwa mara kwa mara wakifunga peke yao, kwa ajili ya afya ya mtoto wao na kwa ajili ya mabadiliko katika ratiba ya kazi ambayo ingeweza kuruhusu Kong Kuk-Won kuhudhuria kanisa. Baada ya mwenzi wangu na mimi kuungana nao katika kufunga, maombi yetu yalijibiwa na ratiba ya kazi ya Kong Kuk-Won ikabadilika. Lakini Pak Mi-Jung alikuwa bado mgumu kuhusu kubatizwa.

Wazo lenye Maongozi

Mwenzi wangu basi alikuwa na wazo jingine zuri. Yeye alitoa nje kitabu chake cha nyimbo cha mfukoni na kuuliza kama tunaweza kuimba pamoja nao. Ingawa sisi tuliwahi kuimba pamoja kwenye hafla ya awali, sijawahi kuona Pak Mi-Jung akiimba na nilidhania tu kwamba yeye hakuwa akipenda kuimba au alikuwa na wasiwasi kwa sababu wimbo ulikuwa mpya kwake. Mwenzangu alimuuliza kama alikuwa na wimbo alioupenda, na kwa kushtuka kwangu, alipaliwa na mate na kujibu kwamba tangu alipokuwa msichana mdogo, wimbo alioupenda ulikuwa “Nina Haja Nawe Kila Saa” (Hymns, no. 98). Tulianza kuimba kwa sauti nne kwa mpangilio, na baba akiimba melodi, mama akiimba alto, na mwenzangu akiimba tena, na mimi nikiimba bezi.

Roho alikuwa na nguvu katika chumba hicho. Tulipoimba aya ya tatu, hisia ilimshinda, na sauti yake ilipungua tulipoendelea:

Nina Haja Nawe Kila Saa,

Kila Hali.

Maisha ni bure,

Usipokuwepo.

Yesu Nakuhitaji;

Vivyo kila saa!

Nibariki, Mwokozi

Nakujia!

Tulipomaliza ubeti wa nne na wa mwisho, yeye alikuwa analia. Mumewe alikuwa anajaribu kumfariji, hatimaye aliweza kujimudu mwenyewe. Yeye alinitazama moja kwa moja machoni na akasema, “Nina haja ya kubatizwa.”

drawing of woman holding an Asian hymnbook

Ibada hii ya ubatizo wa Kong Kuk-Won na Pak Mi-Jung Jumapili ile mchana ilikuwa moja ya ibada za kiroho zaidi katika kazi yangu. Watoto wao walishiriki katika mpango, na waumini mbalimbali wenyeji walihudhuria ili kuonyesha kuunga mkono familia hii mpya iliyoongoka katika kata yao. Mwenzi wangu na mimi tuliimba muziki maalum: “Nina Haja Nawe Kila Saa.”

Hatimaye mimi nilimaliza misheni yangu na kurudi nyumbani. Baada ya mwaka mmoja katika chuo, mimi nikarudi Korea kwa ajili ya kazi ya kupata ujuzi ya majira ya kiangazi, na kila mwisho wa wiki mimi nilichukua hatua ya kuwatembelea marafiki wengi maalum na familia nilizokuwa nimekutana nazo katika misheni yangu. Baada ya wiki chache mimi nilirejea tena Balsan na nilikutana na familia hii maalumu. Baada ya kuwasili katika nyumba yao, mimi niliona kuwa kuna mtu alikuwa amekosekana—mwana wao. Pamoja na machozi katika macho yake, Pak Mi-Jung aliniarifu: saratani ya mwana wao ilirudi na, katika umri wa miaka 14, alikuwa amepoteza pambano.

Nilipokuwa nikijaribu kutoa rambirambi zangu na pia kukabiliana na uchungu niliokuwa nikiusikia, Kong Kuk-Won alinihakikishia mimi kwamba kila kitu kitakuwa SAWA. Waliipenda injili, walihudhuria kanisa kwa uaminifu wakiitazamia siku ile familia yao itakapopata kuunganishwa milele katika Hekalu la Seoul Korea. Licha ya maumivu ya moyoni ambayo wao waliyasikia, familia ilijua kuwa wangeweza tena kuonana na Kong Sung-Gyun na kuwa pamoja tena. Pak Mi-Jung pia aliniambia kuwa kuimba nyimbo za kila siku kulimsadia yeye kupata nguvu ya kuendelea kuishi na kusikia amani inayoambatana nayo ambayo Roho huileta.

Nilipokuwa nikiondoka nyumbani kwao jioni ile, nilitafakari juu ya maneno ya wimbo wa Pak Mi-Jung. Ninashukuru kwamba Baba wa Mbinguni aliibariki familia kwa amani baada ya kufariki kwa Kong Sung-Gyun, na mimi hasa nashukuru kwa nafasi ya Roho Mtakatifu katika kuongoka kwa Pak Mi-Jung, ambako kumeiwezesha familia kufuzu kupata baraka za milele za hekaluni.