2019
Kofia Nyeupe kwa ajili ya Florence
Oktoba 2019


Kofia Nyeupe kwa ajili ya Florence

Mwandishi anaishi Michigan, Marekani.

Picha
A White Cap for Florence

Florence Onyejekwe mwenye miaka kumi na tatu alifika kwenye sehemu yake ya kawaida ndani ya soko lenye watu wengi huko Onitsha, Nigeria. Mtaa ulikuwa umejaa wachuuzi wakiwaita wanunuzi wenye shughuli nyingi. Wanawake wakiwa na mizigo iliyokaa vizuri bila kushikiliwa vichwani wakati wakitembea. Shule ilikuwa imefungwa kwa ajili ya likizo, na Florence alijua rafiki zake walikuwa wakifurahia mapumziko. Lakini Florence alitumia likizo yake kwa kuuza majani machungu hapa sokoni. Ilikuwa ndiyo njia pekee ya kupata fedha kwa ajili ya ada yake ya shule.

Florence hata hivyo hakulalamika. Hata hivyo, mama yake alitumia masaa mengi sokoni kila siku akiuza viazi vitamu ili kununua chakula kwa ajili ya familia. Mama alifanya kazi kwa bidii kubwa. Wazazi wake wote walifanya hivyo. Lakini bila elimu ya kutosha, kulikuwa tu na mengi wangeweza kufanya. Florence alikuwa karibu kumaliza elimu yake ya msingi. Pengine ikiwa angeendelea na shule, angeweza kupata kazi ambayo ingemlipa vizuri na kusaidia familia yake.

Wakati aliporudi nyumbani, Florence aliwakuta wazazi wake na kuwauliza, “Je, mnadhani ningeweza kwenda shule ya sekondari? Na labda chuo kikuu?”

Mama alimtazama Nnam (baba) na kutikisa kichwa chake. “Chuo Kikuu kinahitaji pesa nyingi kuliko kiasi tulichonacho,” alisema Nnam. Florence alitazama chini kwenye viatu vyake. Hakutaka Mama na Nnam kuona jinsi alivyokatishwa tamaa.

Siku chache baadaye, Florence alipita hospitali kuchukua dawa. Hospitali ilikuwa na shughuli nyingi kama vile sokoni, japokuwa hazikuwa na kelele. Florence alikodolea macho wauguzi waliovaa kofia ngumu, nyeupe. Alijiona mwenyewe ndani ya sare kama ile, akiwasaidia wagonjwa na kuwashughulikia watoto katika hospitali kubwa. Pengine yeye angeweza kuwa muuguzi.

Florence alijua wazazi wake walikuwa sahihi—kupata elimu kungekuwa vigumu. Lakini Florence alijua jinsi ya kufanya kazi kwa bidii. Aliamua kujaribu.

Licha ya shughuli nyingi zilizoijaza siku yake, Florence alitenga muda wa kusoma. Alifaulu majaribio ya shule ya sekondari, na Nnam alikopa pesa za kutosha kwa ajili yake kwenda. Baadaye alikuta kwamba serikali ingesaidia kulipia shule ya uuguzi. Ndoto zake zilikuwa zinaweza kufikika!

Lakini ilipofika wakati wa kuanza shule ya uuguzi, Florence alihisi shaka kidogo. Vipi kama ingekuwa ngumu sana? Vipi kama angekuwa mpweke? Florence aliinamisha kichwa na kuomba, “Mungu Mpendwa, tafadhali nipe nguvu za kwenda shule ya uuguzi na kufanya kazi kwa bidii.”

Kwenye shule ya uuguzi, Florence alijifunza jinsi ya kutoa dawa na kuweka vifaa safi kutokana na bakteria. Wakati mwingine wagonjwa wake walipata nafuu, lakini wakati mwingine hawakupata nafuu. Florence aliomba mara kwa mara kwa ajili ya ujasiri. Baada ya miaka mitatu mirefu, Florence alihitimu akipata zawadi ya mwanafunzi bora katika darasa lake. Ndoto yake ilikuwa imetimia! Alipaswa kuvaa kofia nyeupe ya uuguzi, na aliweza kupata kipato cha kutosha kuisaida familia yake.

Miaka mingi baadaye, Florence alizuru tawi dogo huko misheni ya Ghana Accra. Mume wake, Christopher Chukwurah, alikuwa rais wa misheni huko. Florence alikutana na baadhi ya watoto katika tawi lake ambao mara zote hawakwenda shule. Hawakuwa na uhakika nini cha kufanya kwa ajili ya wakati wao ujao. Walimkumbusha Florence kuhusu yeye wakati alipokuwa mtoto. “Nini ninaweza kusema ili kuwasaidia?” Florence aliomba kimya kimya.

Kisha akahisi msukumo dhahiri: Waambie kuhusu maisha yako.

Florence alifikiria kuhusu maisha yake. Alikuwa amefanya kazi hospitalini huko Nigeria na Marekani. Alikuwa ameolewa na mwanaume mzuri, na kwa pamoja walikuwa wamepata Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Alikuwa amekuwa mama. Sasa alikuwa akiwasaidia wamisionari kuwa wenye afya na kufanya kazi kwa bidii. Baba wa Mbinguni alikuwa amemsaidia kuwa muuguzi. Alimwezesha kufanya mengi zaidi ya alivyofikiria. Angeweza kufanya vivyo hivyo kwa watoto hawa.

Florence aliwaangalia watoto na kutabasamu. “Unajua zile kofia nyeupe ambazo wauguzi huvaa? Niliona kofia kama ile na kuamua kuwa muuguzi …”

Chapisha