2019
Changamoto ya Hekalu
Oktoba 2019


Changamoto ya Hekalu

“Mioyo ya watoto itawageukia baba zao” (Mafundisho na Maagano 2:2).

Picha
The Temple Challenge

Jumapili moja mimi na washauri wangu tulizuru mkutano wa Kanisa. Tulitoa mahubiri kuhusu hekalu na mambo maalumu yanayotokea pale. Baada ya mkutano mvulana wa miaka 12 aliyeitwa Colby alikuja kwangu na kunisalimia kwa mkono. Tulipiga domo kuhusu hekalu. Kisha nilimpa changamoto ya kutafuta jina la familia ili kulipeleka hekaluni.

Muda mfupi baadaye, nilipata barua kutoka kwa Colby. Hapa kuna kile Colby alichoniambia:

“Nilikwenda nyumbani na kupata jina jipya. Ilitokea kwamba nilimpata babu yangu-mkuu wa tatu!

“Muda mfupi baadaye nilikwenda hekaluni na kubatizwa kwa ajili yake. Ilikuwa kweli maalumu kwa sababu kaka yangu aliweza kunibatiza na baba yangu aliweza kunithibitisha kwa ajili ya babu.

“Nilipata hisia nzuri za ndani ambazo zilileta amani. Nilihisi kama kile nilichofanya kwa ajili ya babu yangu kilikuwa kizuri hasa kwa sababu sasa anaweza kwenda kwenye ufalme wa selestia kuishi pamoja na familia yake. Kwa siku yote hiyo, nilikuwa na hisia nzuri sana za ndani.

“Niligundua pia kwamba hakuna anayewafahamu wazazi wa babu yangu mkuu wa tatu, hivyo ninaweza kutafuta majina yao na kuyapeleka hekaluni pia!”

Colby ni mfano mzuri kiasi gani wa kuonekana! Bila kujali una umri gani, unaweza kuwa mfano kwa familia yako na rafiki zako. Unaweza kushiriki injili na kila mtu unayemfahamu—hata mababu zako!

Chapisha