2019
Halo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo!
Oktoba 2019


Halo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo!

Hello from the Democratic Republic of the Congo

Habari, Sisi ni Margo na Paolo!

Tunatembelea Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, au D. R. Congo.

D. R. Congo iko Afrika ya kati. Takriban watu milioni 80 wanaishi huko.

Sehemu kubwa ya D. R. Congo imefunikwa na misitu ya mvua. Ni nyumbani kwa wanyama wa kuvutia wa aina mbalimbali, kama vile tembo, sokwe, na faru. Mnyama huyu anaitwa Okapi.

D. R. Congo inajulikana kwa utamaduni wake mzuri wa sanaa, ikijumuisha sanamu za mbao, vikapu vya kusukwa, na barakoa.

Wamisionari kutoka kanisa letu walianza kufundisha watu katika D. R. Congo mnamo 1986. Sasa takriban watu 60,000 huko ni waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Katika D. R. Congo, watu wengi wanazungumza Kifaransa kanisani. Hiyo ndiyo lugha rasmi ya nchi. Lakini kuna lugha zingine takriban 250 zinazozungumzwa huko D. R. Congo!

Mwaka huu, D. R. Congo ilipata hekalu lake la kwanza! Waumini wa Kanisa huko wanafurahi kuwa na hekalu katika nchi yao.

Asante kwa kutalii D. R. Congo pamoja nasi. Tutaonana wakati mwingine!