2019
Safari za Umisionari za Paulo
Oktoba 2019


Hadithi za Maandiko

Safari za Kimisionari za Paulo

Picha
Paul on a boat

Baada ya Yesu kufufuka, Mtume Paulo alisafiri kwenda miji mbalimbali kuwafundisha watu kuhusu Yesu. Hakukuwa na magari wala ndege kipindi hicho, hivyo alitembea sana! Wakati mwingine alisafiri kwa mashua.

Picha
Paul teaching

Paulo aliwafundisha watu makanisani na nyumbani. Alifundisha watu juu ya vilele vya miamba na mitaa ya mji.

Picha
Paul in prison

Watu wengi hawakupenda kile Paulo alichofundisha. Wakati mwingine Paulo alifungwa gerezani. Wakati mwingine Paulo aliugua.

Picha
Paul smiling

Lakini katikati ya magumu haya yote, Paulo alikuwa na imani. Alisema, “Nayaweza mambo yote katika Kristo.” Alijua Mungu angemsaidia kuwa imara.

Picha
girl riding bike

Yesu Kristo anaweza kunisaidia kuwa imara pia. Yeye ananipenda, nami ninampenda Yeye!

Chapisha