2019
Takdiri ya Kiungu
Oktoba 2019


Takdiri ya Kiungu

Mwandishi anaishi Ufaransa.

Rafiki yangu daima alikuwa na furaha muda wote. Ni nini kingeweza kumuudhi?

girls under umbrella

Kielelezo na Reginald Swinney

Natokea Ufaransa, lakini mimi na dada yangu tuliishi kwa mwaka mmoja mashariki ya Marekani kama wanafunzi wa kubadilishana. Kipindi hicho, tulikutana na watu wengi lakini mmoja ambaye aliacha msukumo mkubwa kwangu alikuwa msichana aliyeitwa Destiny. Alikuwa mmoja wa marafiki zangu niliowapenda zaidi. Tulifanya mambo mengi pamoja, wakati wa shule na baada ya shule na pamoja na dada yangu. Destiny daima alikuwa mwenye furaha. Hicho ndicho kitu nilichopenda zaidi kwake.

Kisha siku moja nilimuona katika hali ya wasiwasi ambayo sikuwahi kumuona nayo kabla. Nilimwuliza nini lilikuwa tatizo. Alisema hakupenda kuliongelea. Kisha niliona karatasi mkononi mwake. Niliichukua na kuisoma.

Mtu fulani alikuwa amemwandikia vitu vibaya visivyoaminika. Ujumbe wa siri ulisema alikuwa mbaya, kwamba hakuna aliyempenda, kwamba hakuwa na lengo lolote la kuwa hai, na kwamba alipaswa kujiua. Sikuweza kuamini mtu kama yeye angeweza kushambuliwa vile. Iliniathiri sana kujua maumivu aliyokuwa akipitia.

Tangu hapo, nilifanya juhudi kubwa zaidi kuwa rafiki wa Destiny—si tu kutumia muda pamoja naye, bali daima kuwepo kwa ajili yake, na hasa kuwa mkweli. Nilimwelezea kwamba yeye alikuwa binti wa Mungu, aliyebarikiwa na asili takatifu, aliyestahili kupendwa na mwenye uwezo wa mambo makubwa.

Ni vigumu kujaribu kujipenda mwenyewe wakati wengine wanapokutendea vibaya na kukukosoa. Nilipokuwa na urafiki na Destiny, nilijifunza kuwa wakati mwingine njia nzuri ya kuwasaidia wengine ni kuwapenda tu na kuwasaidia kujua wao ni akina nani hasa.

Mwishoni mwa mwaka, nilipopaswa kurudi Ufaransa, Destiny aliniambia jambo ambalo daima nitalithamini. “Emma,” alisema, “umeniokoa. Kabla hujaja, nilitaka kujiua. Lakini wewe na dada yako mmenisaidia sana, kwa kujali tu. Leo ninajipenda, na ninawapenda.”

Kuna watoto wengi shuleni wanaovumilia ukatili, ambao wanatendewa vibaya au kutengwa. Tafuta njia ya kuwafikia. Zungumza nao, wafikirie, kuwa mkarimu kwao. Ndicho ambacho Mwokozi angefanya, na wakati mwingine kusema tu halo au kutabasamu kunaweza kubadili kila kitu.