2019
Wilson Di Paula—San José, Uruguay
Oktoba 2019


Taswira za Imani

Wilson Di Paula

San José, Uruguay

Picha
Wilson and his daughter sitting at home

Ajali ya pikipiki ilimuacha Wilson akiwa amepooza. Mwaka mmoja baadaye mkewe akafariki. Kama mjane mwenye watoto wawili wadogo wa kike, Wilson hakujua nini cha kufanya. Hakujua ikiwa kulikuwa na lengo katika maisha. Wilson angeweza kuwa mkali. Badala yake, alianza kutafuta ukweli.

Cody Bell, mpiga picha

Baada ya ajali ya pikipiki na kumpoteza mke wangu, nilibaki na watoto wawili wadogo wa kike kuwalea. Sikujua hasa jinsi ambavyo ningewalea mabinti zangu kwenye kiti cha walemavu. Ajali hii ilibadili maisha yangu kabisa.

Nilikuwa na maswali mengi. Kwa nini mambo mabaya hutokea? Nilikuwa nikienda wakati wote nikijaribu kufanya mambo sahihi, na mke wangu alichukuliwa kutoka kwangu na niliachwa kwenye kiti cha walemavu, kisha madaktari walitakiwa kumfanyia upasuaji wa kichwa binti yangu ili kuondoa uvimbe. Nilianza kufikiri kwamba hakukuwa na lengo katika maisha.

Nilitambua kwamba nilihitaji kupata ukweli. Nilichunguza madhehebu tofauti na kupata Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Nilihisi kwamba lilikuwa ni ukweli.

Nilijifunza kwamba kuna maisha baada ya haya, na tunapokufa, inawezekana kuwa na wale tunaowapenda. Hii iliniletea furaha kwa sababu ya miaka 10 ya kupendeza ambayo nilikuwa nimekuwa nayo pamoja na mke wangu.

Kupata injili kulibadili maisha yangu kwenye kila hisia. Nilianza kupata amani ya akili na amani ya nafsi. Furaha iliingia kwa familia yangu pale tulipokwenda kanisani kila Jumapili. Tulirudi nyumbani tukiwa tumeimarishwa. Tulibatizwa na hatimaye kuunganishwa kwa milele yote ndani ya hekalu huko Argentina.

Sasa ninaendelea kusonga mbele Kanisani. Nimetumikia kama mshauri katika uaskofu, na ninajaribu kujifunza kutokana na uzoefu wangu wote, kutokana na majaribu yote ya maisha. Hii hunipa nguvu. Wakati nimekuwa kwenye kiti cha walemavu kwa zaidi ya miaka 20, nimejifunza kwamba furaha huja kutoka ndani. Mtu hujifunza zaidi kila siku. Kwa hilo ninahisi shukrani.

Sasa ninajua kwamba kuna lengo la kuwa hapa duniani. Tuko hapa kama sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni. Tunaye Mwokozi ambaye alishinda kifo na alifufuka. Kujua hili kunanipa nguvu. Sasa, ninajitahidi kuvumilia na kusonga mbele. Nina lengo na ninajua kwamba pale ninapojaribu kuishi maisha ya kustahili, ninaweza kuwa na familia ya milele.

Picha
Wilson next to a window while Sofia looks on

Licha ya changamoto ambazo Wilson na binti yake Sofia wanakabiliana nazo, injili inawapa amani, furaha, na nguvu. Sofia ameishi na baba yake tangu upasuaji wake. Wilson anapata furaha kwa kutumikia Kanisani.

Picha
Wilson in the kitchen

Kupika wakati akizungusha kiti chake kuzunguka jikoni ni moja ya ujuzi mwingi Wilson aliojenga tangu ajali ilipomwacha akiwa amepooza.

Picha
Wilson studying the scriptures

Wilson anapata tumaini na nguvu kutoka kwa Mwokozi wakati anaposoma maandiko.

Picha
missionaries praying with Wilson and his daughter at the table

Wamisionari wanaungana na familia ya Di Paula kwa ajili ya chakula cha jioni. Upendo wa Wilson wa injili ni nguvu kwa familia yake na kwa Kanisa.

Picha
Wilson looking out a window

Baada ya ajali mbaya na kifo cha mkewe, Wilson alitia shaka lengo la maisha. Alipata lengo wakati alipopata injili ya Yesu Kristo.

Picha
Wilson at the doorway while his daughter walks outside holding dogs

Wilson na Sofia wanapata tumaini kwenye injili. Kukaa kwa zaidi ya miaka 20 kwenye kiti cha walemavu hakujamzuia Wilson kutumikia katika njia zenye maana.

Picha
Wilson smiling while daughter stands nearby

Tabasamu la Wilson linatoa ushahidi wa wingi wa mambo ya kiroho katika maisha yake. “Furaha huja kutoka ndani,” Wilson anasema. “Mtu hujifunza zaidi kila siku.”

Picha
missionaries eating dinner with Wilson and his daughter

Wakati wanapokula pamoja, familia ya Di Paula inashiriki zaidi ya chakula pamoja na wamisionari, wanashiriki pia upendo wao na shukrani kwa ajili ya injili.

Chapisha