2019
Kuwapenda Wengine kama Yesu Anavyotupenda
Oktoba 2019


Kutoka kwa Urais wa Kwanza

Kuwapenda Wengine kama Yesu Anavyotupenda

Imetoholewa kutoka “Kuwapenda Wengine na Kuishi kwa Utofauti,” Liahona, Nov. 2014, 25–28.

Picha
Loving Others as Jesus Loves Us 1
Picha
Loving Others as Jesus Loves Us 2

Yesu aliwapa wafuasi wake amri kuu: “Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi” (Yohana 15:12). Kama wafuasi wa Kristo, tunapaswa kuishi kwa amani na wengine. Hiyo hujumuisha watu ambao hawaamini mambo sawa na yale tunayoamini.

Hapa kuna baadhi ya njia tunazoweza kuwapenda wengine kama Mwokozi anavyotupenda:

  • Kuwa mkarimu kwa watu ambao wako tofauti.

  • Onyesha heshima kwa imani zao.

  • Kamwe usimuonee au kumtukana yeyote.

  • Kuwa msikilizaji mzuri.

  • Kuwa mpole. Usibishane kwa hasira.

  • Simamia kwenye kilicho kweli.

  • Waambie wengine kuhusu injili kwa njia ya unyenyekevu. “[Zungumza] ukweli katika upendo” (Waefeso 4:15).

Amri ya Mwokozi wetu ya kupendana kama Yeye anavyotupenda pengine ni changamoto yetu kuu. Ninaomba kwamba tuweze kujaribu kuonyesha upendo katika yote tunayofanya.

Chapisha