Liahona
Russell M. Nelson: Nabii kwa ajili ya Siku Yetu
Septemba 2024


Russell M. Nelson: Nabii kwa ajili ya Siku Yetu, Liahona, Septemba 2024.

Russell M. Nelson: Nabii kwa ajili ya Siku Yetu

Tukiwa na nabii wa kutuongoza katika hizi siku za mwisho, kwa kweli sisi ni watu walio barikiwa.

Rais Nelson akisalimiana na watu

Rais Russell M. Nelson anasalimiana na watu baada ya mkutano wa ibada huko Singapore mnamo Novemba 28, 2019.

Wakati msaili alipokosoa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kama “kanisa linaloongozwa na wanaume wazee,” Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) alijibu, “Si inapendeza kuwa na mtu aliyekomaa kama kiongozi, mtu wa maamuzi ambaye hawezi kuyumbishwa na kila upepo wa mafundisho?”

Rais Russell M. Nelson, nabii aliye hai mzee zaidi kuhudumu katika kipindi hiki, ni mtu wa namna hiyo. Anakamilisha mwaka wake wa 100 ifikapo Septemba 9, 2024. Ni kiongozi mwenye huruma ya ajabu na utambuzi, maono na mchangamfu, mwenye moyo mkunjufu na hekima.

Nampenda Rais Nelson. Tumekuwa marafiki kwa miaka 60 na mtume mwenza kwa miaka 40. Tangu Januari 2018, nimebarikiwa kuhudumu chini ya maelekezo yake katika Urais wa Kwanza wa Kanisa.

Aliitwa kuongoza Kanisa la urejesho la Yesu Kristo na kuwa mwalimu mahiri, Rais Nelson anamjua Mwokozi, ambaye yeye ni nabii Wake. Kupitia karne ya kuishi na kujifunza, yeye amebobea katika taaluma na huduma ya kijeshi Akiwa na familia kubwa, yeye amekuwa kiongozi wa familia mwenye upendo na mwenye ufanisi. Kupitia miito ya Kanisa, ikijumuisha miaka sita iliyopita kama nabii wa Bwana, yeye amekuwa kiongozi wa mfano wa kuigwa katika Kanisa la Bwana lililorejeshwa.

Rais Russell M. Nelson

Kupitia karne ya kuishi, Rais Nelsona amejifunza na kutumia funguo za furaha katika maisha haya na katika maisha yajayo—kile alichokiita “masomo muhimu sana” ya maisha,”

Ametufunfdisha kwamba tunapaswa “kuanza na mwisho akilini.”

Anaipenda nyumba ya Bwana. Wakati wa miaka yake kama Rais wa Kanisa, yeye ametangaza mahekalu 153 mapya—karibu nusu ya jumla ya mahekalu 335 ya Kanisa ambayo yamejengwa, yako katika hatua za ujenzi, au yametangazwa katika kipindi hiki.

Ametuambia sisi kwamba ujenzi wote wa mahekalu yetu ni kuleta hekalu, na baraka za maagano ya hekaluni, karibu zaidi na watoto wa Mungu. Huo ndio mpango wa Mungu.

Rais Nelson amefundisha, “Nimejifunza kwamba mpango wa Baba wa Mbinguni kwetu ni wa kupendeza zaidi, kwamba tunachokifanya kwenye maisha haya kina umuhimu sana, na kwamba Upatanisho wa Mwokozi ndio unaoufanya mpango wa Baba kuwezekana.” Uelewa wa mpango huu, yeye alisema “huondoa dukuduku za maisha na shaka juu ya siku zetu za usoni. Huturuhusu kila mmoja wetu kuchagua jinsi tutakavyoishi hapa duniani na mahali tutakapoishi milele.”

Kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, sisi ni watu walio barikiwa kuongozwa na mtumishi mnyenyekevu wa Bwana, Rais Nelson, ambaye amejitolea kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi wetu na Mkombozi wetu, Yesu Kristo. Na sisi sote tuendelee kusali kwa ajili yake, kushuhudia juu yake, kumkubali, na kumshukuru Mungu kwa ajili ya nabii wetu—Rais Russell Marion Nelson.