“Kupata Faraja katika Uhusiano Wetu wa Agano na Mungu,” Liahona, Septemba 2024.
Kupata Faraja katika Uhusiano Wetu wa Agano na Mungu
Yesu Kristo ndiye kiini cha upendo safi, uponyaji, furaha, na faraja.
Kupata Faraja kupitia uhusiano wetu wa agano na Mungu imekuwa akilini mwangu na moyoni mwangu kwa muda fulani. Kama vile nabii wa Bwana alivyofundisha na kutusihi tujifunze kuhusu maagano, mahekalu, na nguvu za ukuhani, nimejikuta mwenyewe nikipekua, nikipenda na nikisherekea ukweli wenye kurudisha nguvu mseto zilizo ndani ya maagano.
Tulikusudiwa kuwa na ubia na Bwana katika njia yenye nguvu kupitia maagano yetu. Yeye anatamani kuwa pamoja nasi katika wasiwasi wetu na maamuzi yetu. Hatuhitaji kupitia changamoto, huzuni, kutokujiamini, na maumivu ya maisha peke yetu. Yeye atakuwa kando yetu. Yeye alisema, “Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.” (Yohana 14:18).
Rais Russel M. Nelson alielezea sifa ya Mungu na upendo Wake mkuu kwa ajili yetu wakati alipofundisha kwamba “njia ya agano ni kuhusu tu uhusiano wetu na Mungu.” Yeye alisema: “Mara wewe na mimi tukiwa tayari tumefanya agano na Mungu, uhusiano wetu na Yeye unakuwa wa karibu zaidi kuliko kabla ya agano letu. Sasa tumeunganishwa pamoja. Kwa sababu ya agano letu na Mungu, Yeye kamwe hatachoka katika juhudi Zake za kutusaidia sisi, na kamwe sisi hatuwezi kumaliza subira Yake yenye rehema kwetu. Kila mmoja wetu ana sehemu maalum katika moyo wa Mungu. Yeye ana matumaini makubwa kwetu sisi.”
Chanzo Changu Kikuu cha Amani
Kama dada ambaye bado sijaolewa, uhusiano huu wa agano wa upendo na rehema na Baba yangu aliye Mbinguni na Mwokozi una mahali pa nguvu katika maisha yangu na umekuwa na ni chanzo changu kikuu cha faraja na amani. Bila kujali hali zetu za ndoa au asili, Bwana anatamani sisi tuwe na ubia na Yeye katika njia yenye nguvu—tuwe “kitu kimoja” (3 Nefi 18:23) pamoja na Yeye katika “matendo [yetu] yote” (Alma 37:37). Tunapomlilia Bwana kwa ajili ya usaidizi wetu, na “acha mapenzi ya mioyo [yetu] yaelekezwe [Kwake] milele” (Alma 37:36; msisitizo umeongezwa), maisha yetu yanaweza kujazwa na muunganiko huu mzuri wa agano.
Kupitia Mwokozi wetu, Yesu Kristo, tunaweza kupata faraja kutokana na kupitia changamoto za maisha peke yetu.
Sisi sote tuna mashaka na shida ambazo tunaweza kuhisi kuwa peke yetu kwazo. Yeye anajali kuhusu mashaka yetu bila kujali jinsi yalivyo makubwa au madogo. Nimeshisi hitaji la msaada Wake wakati nikiwa na wasiwasi kuhusu mambo yanayoweza kuonekana kuwa madogo kama vile rafiki wa muda wote niniyempa jina “mrekebishaji wa nyumbani.” Bila mwenza wa kushauriana naye, ninaweza kuwa na mashaka peke yangu kuhusu mkandarasi sahihi, gharama nafuu, kuomba ruhusa kazini ili niwe nyumbani, na kuwa msimamizi mzuri wa fedha zangu na nyumba yangu. Ilikuwa ni ushindi siku moja kuweza kufanikisha mlango wa gereji yangu kurekebishwa! Bwana alisikia wasiwasi wangu. Na ingawa ni kitu kidogo katika ukubwa wa mambo, Yeye alijibu sala zangu. Kwa jinsi gani? Kupitia jirani mkarimu, msaada wa Roho, na video ya YouTube, nilibarikiwa kujua nini cha kufanya ili kurekebisha mlango.
Kama Bwana ni msikivu kwa mahitaji madogo, hebu fikiria tamanio Lake kutubariki na kutusaidia sisi katika masuala mazito ya moyo na nafsi, ambayo si machache kwa idadi: unyanyasaji, uraibu, uhusiano mgumu wa kifamilia, upotevu na kuvunjika moyo, changamoto endelevu za afya ya kiakili na kimwili, dhiki ya kifedha, wasiwasi kila mara kama mzazi, wasiwasi kila mara wa kumtunza mzazi, mapambano binafsi ya kiimani, mtoto au mwenza ambaye anachagua kutoshiriki katika injili.
Wakati wa ukali na udhaifu wa maisha, nimetegemea sana juu ya na kukumbatia uhusiano wangu wa agano na Mungu. Wakati nilipotumainia katika utunzaji wa upendo wa Mungu na kujaribu niwezavyo kuweka wakfu maisha yangu Kwake, Yeye amenipatia faraja kupitia nguvu Zake za ukuhani na amekuwa Mtoaji wangu katika mahitaji yangu ya kiroho na kimwili. Yeye ametoa faraja kutokana na hofu, faraja kutoka na kutojiamini, faraja kutokana na kiburi, faraja kutokana na dhambi, faraja kutokana na upweke, faraja kutokana na huzuni.
Rais Nelson alifundisha kwa uwazi na hakikisho kwamba “thawabu ya kushika maagano na Mungu ni nguvu ya mbinguni—nguvu ambayo inatuimarisha ili tustahimili majaribu yetu, vishawishi na maumivu yetu ya moyo vyema zaidi.”
Kupitia Yesu Kristo, sisi tunaweza kupata faraja kutokana na kupitia changamoto za maisha peke yetu.
Akina dada “juu ya Visiwa vya Bahari”
Wakati nimekuwa nikitafakari juu ya baraka muunganiko wa agano tulionao kwa Mungu, nilifikiria kuhusu jukumu langu la kutembelea Eneo la Asia ya Kaskazini.
Nilipata fursa ya kusafiri hadi kwenye visiwa vidogo vya Chuuk huko Micronesia, karibia maili 1,500 (kilomita 2,400) kusinimashariki mwa Japani. Wawili kati ya akina dada huko Weno, Chuuk, walikuwa wamejitolea maisha yao kuwalea watoto ambao walikuwa wametelekezwa na wazazi wao. Akina dada hawa wawili walihisi ilikuwa ni muhimu kuwalea watoto hawa katika injili. Mmoja wa akina dada hawa ni mseja na anafanya kazi kama mshauri shuleni.
Nilishiriki na wao ujumbe wa Rais Nelson kwa akina dada wa Kanisa, ambao ni kwamba ninyi akina dada mnapendwa, ni wa muhimu, na ni wenye thamani.
Dada mseja mrembo ambaye anawalea binamu zake wa kike na kiume alibubujikwa na machozi na kusema yeye hajahisi kuwa mwenye thamani hivi karibuni; alihisi kusahauliwa. Lakini alishuhudia alihisi upendo wa Mungu na kujulikana kwake katika maneno ya nabii kwamba yeye kwa kweli alikuwa wa “thamani,” na alijua ilikuwa ni kweli. Alihisi upendo wa uponyaji wa Mungu, alihisi faraja.
Bwana amesema, “Je, hujui kwamba Mimi, Bwana Mungu wako, nimeumba wanadamu wote, na kwamba nawakumbuka wale ambao wako juu ya visiwa vya bahari?” (2 Nefi 29:7).
Akina dada hawa wanajulikana kwa Baba yao wa Mbinguni na Mwokozi. Hawako peke yao. Na ndivyo ilivyo kwako wewe na mimi katika majaribu yetu na changamoto zetu. Bwana alinituma mimi karibia maili 8,500 (kilomita 13,700) kwa ndege, gari moshi, gari, na mashua ili kuleta upendo wa Mungu na faraja kwa “wale” walio juu ya visiwa vya bahari. Na Yeye vivyo hivyo atakupata wewe na mimi juu ya visiwa vyetu binafsi pale ambapo tungeweza kuhisi kuwa peke yetu katika wasiwasi na mizigo tunayobeba katika mioyo yetu. Yeye yupo hapo na amejiandaa kutubariki, kutuongoza, na kutufariji.
“Ninaweza Kuja Kwako”
Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) wakati mmoja alielezea uzoefu wa mama kijana aliyetalikiwa “mama wa watoto saba bado wakiwa na umri wa kutoka miaka 7 hadi 16. Yeye alisema kwamba jioni moja alivuka mtaa ili kumpelekea jirani kitu fulani.” Haya ni maneno yake kama anavyoyakumbuka:
“Nilipogeuka kutembea kurudi nyumbani, niliweza kuona nyumba yangu imewashwa taa. Niliweza kusikia mwangwi wa sauti za watoto wangu nilipokuwa nikitembea kutoka mlangoni dakika chache hapo kabla. Walikuwa wanasema: ‘Mama, tunakula chakula gani jioni?’ ‘Unaweza kunipeleka maktaba?’ ‘Ninapaswa kupata karatasi za bango jioni hii.’ Nikiwa mchovu na niliyechoka, nilitazama nyumba ile na kuona taa ikiwaka katika kila chumba. Nilifikiria juu ya hawa watoto wote ambao walikuwa wananisubiri nyumbani ili nije na kukidhi mahitaji yao. Mizigo yangu ilionekana kuwa mizito zaidi kuliko vile ambavyo ningeweza kuibeba.
“Ninakumbuka kuangalia kupitia machozi kuelekea angani, na nikasema, ‘Baba Mpendwa, siwezi kufanya chochote usiku huu. Nimechoka sana. Siwezi kukabiliana na haya. Siwezi kwenda nyumbani na kuwashughulikia watoto hawa wote peke yangu. Naweza tu kuja Kwao na kukaa Nawe kwa usiku huu mmoja tu? …’
Sikusikia kwa kweli maneno ya majibu, lakini niliyasikia katika akili yangu. Jibu lilikuwa: ‘Hapana, mdogo we, hauwezi kuja kwangu sasa. … Lakini Mimi ninaweza kuja kwako.’”
“Ninaweza kuja kwako.” Yeye alikuja kwake, na Yeye atakuja kwako na mimi, kama vile Mwokozi alivyokuja kwa mwamamke kisimani pale alipokuwa anafanya kazi na kuhangaika katika siku zake (ona Yohana 4:3). Yeye alimtia moyo, alimfundisha, alitangaza umasiya Wake kwake, na alimpenda wakati ambapo yeye mwenyewe hakujipenda. Kwa yule mwanamke kisimani, kwa yule mama kijana wa watoto saba, kwako wewe na mimi, Yesu anasimama tayari kutoa faraja, Ninashuhudia kwamba sisi tunaweza kupokea faraja kupitia muunganiko wa agano letu na Mungu mwenye upendo.
Pengine kama vile mimi, umesihi kwa ajili ya msaada wa kutoachwa peke yako wakati wa baadhi ya misimu migumu zaidi ya kihisia, kimwili, na kiroho katika maisha yako. Ukali huu wa misimu ya ukuaji umeacha kile ninachokiita “alama za kunyooshwa kiroho” kwenye nafsi . Lakini ninatoa ushuhuda kwamba Yeye alinibeba mimi, na Yeye atakubeba wewe. Yeye amekuchora katika viganja vya mikono Yake (ona Isaya 49:16; 1 Nefi 21:16). Yeye amekuwa hapo wakati wewe umetafuta “kuwa mwenye haki gizani,” Yeye hajaniacha mimi, wala Yeye hatakuacha wewe. Na mimi nitampenda Yeye milele kwa ajili ya hilo.
Wapendwa dada zangu na kaka zangu, chanzo cha upendo safi, uponyaji, furaha, na faraja kimepatikana katika Yesu Kristo. Ninashuhudia kwamba Yesu Kristo ni faraja.
Yeye anatamani kuwa pamoja wewe, ili kukubariki na kukusamehe. Yeye alikuja kwa ajili ya dhumuni hili hili, kukupa wewe faraja inayohitajika sana ambayo wewe unatafuta. Yeye ndiye Mkombozi wa ulimwengu, na ninashuhudia kwamba Yeye yu hai na Yeye anakupenda.
Kutoka kwenye mahubiri ya mkutano wa Wanawake wa Chuo Kikuu cha Brigham Young iliyotolewa Mei 3, 2023.