2023
Nazi na Zaka
Novemba 2023


“Nazi na zaka,” Rafiki, Nov. 2023, 8–9.

Imeandikwa na Wewe

Nazi na Zaka

Picha
alt text

Mambo! Jina langu ni Avehei. Ninaishi Tahiti. Kwenye kisiwa changu, ninapenda kuwa nje ya nyumba. Napenda kupanda milima na kuogelea katika mto au baharini. Ninapenda pia kufanya mambo pamoja na familia yangu. Ninapenda kupika, kucheza karata na kutembea kupanda milima. Ninapenda kucheza mpira na kaka yangu na binamu zangu.

Wakati wa likizo ya msimu wa kiangazi, ninafanya kazi pamoja na kaka yangu katika kijisitu cha minazi. Tunaokota nazi na kuziweka katika rundo kubwa. Pia tunakusanya majani yaliyodondoka ili kijisitu kibakie safi.

Picha
alt text

Baba wa babu yangu hutulipa tunapofanya kazi katika kijisitu hicho. Daima ninalipa zaka kwa pesa ninayolipwa. Nimejifunza kutoka kwa familia yangu na walimu wa Msingi namna ya kulipa zaka.

Ninalipa zaka kwa sababu ninajua kwamba mimi na familia yangu tunabarikiwa wakati tunapotii. Nimebarikiwa kwa familia yangu, nyumba na ulimwengu mzuri unaonizunguka.

Ninajua kwamba Mungu yu hai na kwamba ananipenda. Ninamshukuru Baba wa Mbinguni kwa familia ambayo Yeye amenipa.

Picha
alt text
Picha
alt text here

Chapisha