2023
Shughuli za Njoo, Unifuate
Novemba 2023


“Shughuli za Njoo, Unifuate,” Rafiki, Nov. 2023, 10–11.

Shughuli za Njoo, Unifuate

Kwa ajili ya jioni ya nyumbani au kujifunza maandiko—au kwa ajili ya burudani tu!

Yesu Kristo Ni Mwongozo Wetu.

Kwa ajili ya Waebrania 1–6

Picha
alt text

Vielelezo na Katy Dockrill

Hadithi ya: Yesu Kristo ni “kapteni wa wokovu [wetu]” (Waebrania 2:10). Kapteni anaongoza meli baharini. Yesu pia anaweza kutuongoza sisi kwenda mbinguni ili tuweze kuishi na Yeye siku moja!

Wimbo: “Ninakuhitaji” (Nyimbo za Dini, na. 47)

Shughuli: Chora picha ya boti ikiwa juu ya mawimbi. Kisha andika au zungumza kuhusu jinsi ambavyo unaweza kumfuata Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani Yeye anakuongoza katika maisha yako?

Mashujaa wa Imani

Kwa ajili ya Waebrania 7–13

Picha
alt text

Hadithi: Maandiko yanasema kwamba imani maana yake ni kuamini katika mambo usiyoweza kuyaona kwa macho (ona Waebrania 11:1). Waebrania 11 inasimulia hadithi ya watu wengi ambao walikuwa na imani. Kuwa na imani katika Yesu Kristo hutupatia sisi amani na ujasiri.

Wimbo: “Faith” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97)

Shughuli: Fanyeni zamu kuchagua shujaa wa andiko kutoka Waebrania 11. Wengine wote waliobaki wanauliza maswali ya kukisia shujaa huyo ni yupi. Je, unawezaje kuwa na imani kama watu katika maandiko haya?

Mtiririko wa Huduma

Kwa ajili ya Yakobo

Picha
alt text

Hadithi: Mtume Yakobo alifundisha kwamba tunapaswa kuwasaidia wale walio katika shida (ona Yakobo 1:27). Je, ni nani anahitaji usaidizi wako?

Wimbo: “When We’re Helping” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198)

Shughuli: Kukimbia! Weka mstari wa kuanzia na wa kumalizia. Kisha songa kwenye mstari wa kumalizia kwa kutelezesha miguu yako mbele bila ya kuinyanyua. Mshindi wa mbio hizo anachagua tendo la huduma ili lifanywe na kikundi chote, kama vile kutuma ujumbe wa ukarimu kwenda kwa mtu fulani au kumtembelea mtu aliye mpweke.

Msaada kwa ajili ya Mababu Zetu

Kwa ajili ya 1 na 2 Petro

Picha
alt text

Hadithi: Mababu zetu wanaweza kujifunza kuhusu injili baada ya kufariki dunia (ona 1 Petro 4:6). Hekaluni tunaweza kubatizwa kwa niaba yao na kuwasaidia wamfuate Yesu Kristo!

Wimbo: “Family History—I Am Doing It” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 94)

Shughuli: Tumia matofali au miche miraba ya miwa ili kujenga hekalu. Je, unawezaje kujiandaa kuingia hekaluni?

Kuonesha Upendo

Kwa ajili ya 1–3 Yohana; Yuda

Picha
alt text

Hadithi: Baba wa Mbinguni anatupenda sisi sote! Mtume Yohana alitufundisha tuwapende wengine pia (ona 1 Yohana 4:19, 21). Je, unawezaje kuonesha upendo kwa wengine?

Wimbo: “Where Love Is” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 138–39)

Shughuli: Funua ukurasa wa 12 ili kufanya shughuli ya kutengeneza mioyo ya karatasi. Kisha wape mioyo hiyo watu uwapendao!

Chapisha