2023
Nini kipo Akilini Mwako?
Novemba 2023


“Nini kipo Akilini Mwako?” Rafiki, Nov. 2023, 38.

Nini kipo Akilini Mwako?

Nahisi kama mengi yanabadilika, na mimi siko tayari. Kwa nini mambo hayabaki vile vile.

—Kukulia huko Granada

Picha
alt text

Kielelezo na Pauline Gregory

Mpendwa Unayekua,

Fikiria kuhusu hadithi yako pendwa isiyo ya kawaida. Mashujaa walikabiliwa na mabadiliko makubwa na changamoto kabla ya kufikia malengo yao, sawa? Kama hakuna kitu kilichobadilika kwao, kusingekuwa na mambo ya kusisimua! Wala mwisho wenye furaha!

Badiliko ni muhimu kwa hadithi yako pia. Kuhisi huzuni, wasiwasi, au kuogopa ni kawaida. Lakini kumbuka kwamba wewe ni shujaa wa hadithi yako. Kila badiliko ni nafasi ya kujifunza na kukua. Na Baba wa Mbinguni atakusaidia.

Uwe na safari njema!

Gazeti la Rafiki

Ingia kwenye kusudio la safari kwa kujichora wewe mwenyewe kama shujaa wa safari!

Chapisha