2023
Kufanya Majaribio
Novemba 2023


“Kufanya Majaribio,” Rafiki, Nov. 2023, 30–31.

Kufanya Majaribio

Jared alijua kwamba Yesu Kristo alikuwa upande wake.

Hadithi hii ilitokea huko Ufaransa.

Picha
alt text

Jared alidunda dunda mpira kuzunguka uwanjani. Wachezaji walikimbia wakimzunguka, viatu vyao vikipiga kelele sakafuni.

“Niko wazi!” Gabriel aliita.

Jared alimpasia mpira Gabriel na akaendelea kukimbia. Kisha Gabriel akapasi mpira ule kwa Jared tena. Jared alirusha mpira ule golini.

SWOOSH!

Umeingia!

“Kazi nzuri, Jared,” kocha wake alisema baada ya mchezo. “Unajua, kufanya majaribio kwa ajili ya timu ya mkoa ni ndani ya wiki mbili.”

Jared alitabasamu. Ni wachezaji wachache tu walikuwa wamealikwa kufanya majaribio kwa ajili ya timu hiyo.

“Kufanya majaribio kutakuwa siku ya Jumapili,” kocha alisema. “Unadhani utaweza kufika?”

Shauku ya Jared ilipotea haraka kama vile ilivyokuja.

“Siku ya Jumapili?” Jared aliuliza.

“Ndiyo. Je, hilo ni tatizo?”

Jared alifikiria kuhusu hilo. Hii ilikuwa nafasi nzuri ya kuchezea timu nzuri! Lakini Jumapili ndiyo siku ambayo alienda kanisani na kufokasi juu ya Mwokozi.

“Jumapili ni siku maalumu kwa ajili yangu mimi,” Jared alisema. “Lakini nitazungumza na wazazi wangu kuhusu hilo.”

Usiku ule, Jared alikaa kitandani kwake pamoja na wazazi wake. Aliurusha ule mpira wa kikapu angani wakati akifikiri. “Hakika ninataka kufanya majaribio kwa ajili ya timu hii,” alimwambia Mama na Baba. “Lakini sitaki kuyafanya siku ya Jumapili. Ninajua Mungu ni muhimu zaidi kuliko mpira wa kikapu.”

“Je, tunaweza kufanya nini ili tusaidie?” Mama aliuliza.

Jared aliugeuza mpira ule mikononi mwake. “Je, tunaweza kusali pamoja?”

Aliuweka ule mpira kando na akapiga magoti pamoja na Mama na Baba. “Mpendwa Baba wa Mbinguni,” alisema, “Ninataka, ninataka sana kufanya majaribio kwa ajili ya timu hii ya mpira wa kikapu. Lakini majaribio ni siku ya Jumapili! Ninajua Jumapili ni siku ambayo ninaitoa Kwako. Je, naweza kufanya nini?”

Baada ya sala, Jared alipata hisia za faraja.

“Je, unahisije?” Mama aliuliza.

“Sitaenda kama majaribio ni siku ya Jumapili,” alisema. “Lakini ninahisi yote yatakuwa SAWA.”

Picha
alt text

Siku mbili baadaye, mama yake Jared alipata barua pepe. Ilisema majaribio sasa yangekuwa siku ya Jumamosi badala ya Jumapili.

Jared angeweza kufanya majaribio na kuitakasa siku ya sabato! Alijua kwamba Baba wa Mbinguni alikuwa amesikia sala yake.

Kwa wiki mbili zilizofuata, Jared alifanya mazoezi ya mpira wa kikapu mara nyingi kadiri alivyoweza. Siku hiyo kubwa ilipofika, Jared alifanya vizuri kadiri alivyoweza. Alikimbia kwa kasi katikati ya mchezo, alirusha mipira mingi golini na aliwashangilia wachezaji wenzake.

“Wachezaji wafuatao wataendelea na kufanya majaribio kwa ajili ya timu,” kocha alisema baada ya mzunguko wa mchezo wa kwanza. “Tafadhali sikiliza jina lako.”

Moyo wa Jared ulidunda kwa kasi. Kocha aliita jina moja. Kisha lingine. Na lingine. Jared alihisi matumaini ya kuwepo katika timu yakianza kufifia.

Mara kocha akawa amemaliza orodha. Hakuwa ameliita jina la Jared. Jared asingeweza kuendelea kuwepo kwenye mzunguko unaofuata wa kufanya majaribio.

Jared alikaa kwenye benchi nje ya jimu na kutolea macho viatu vyake. Alikuwa amefanya kazi kwa bidii. Lakini ilionekana kana kwamba kazi yake yote ilikuwa haina maana.

Mama alipokuja kumchukua, Jared alitikisha kichwa. “Sikufanikiwa kuchaguliwa kwenye timu.”

Mama alimpa kumbatio kubwa. “Pole kwa kutoweza kuchaguliwa kama tulivyotaka,” alisema.

Jared alivuta pumzi ndefu. Kisha wazo la kufariji likamjia.

“Mambo siku zote hayatakuwa jinsi tunavyotaka sisi,” alisema. “Lakini Yesu Kristo anajua jinsi gani ninavyohisi. “Yeye yuko upande wangu.”

Mama alitabasamu. “Uko sahihi! Yeye anajua jinsi unavyohisi.

Jared naye alitabasamu pia. Bado alihuzunika, lakini alihisi vyema kujua Mwokozi alielewa jinsi alivyohisi. Jared alijua Yesu daima atampenda na kumsaidia.

Picha
alt text
Picha
alt text here

Vielelezo na Britain Morris

Chapisha