2023
Akoni Anajitayarisha kwa ajili ya Hekalu
Novemba 2023


“Akoni anajitayarisha kwa ajili ya hekalu,” Rafiki, Nov. 2023, 36–37

Akoni Anajitayarisha kwa ajili ya Hekalu

Kutana na Akoni na jifunze ni jinsi gani alijitayarisha kwenda hekaluni.

Picha
alt text

Akoni ana umri wa miaka 12. Anaishi huko New Mexico, Marekani katika Taifa la Navajo. Hili ni eneo la Marekani linalotawaliwa na watu wa Navajo. Zaidi ya watu 250,000 wanaishi huko.

Picha
alt text

Akoni alipokuwa mdogo, aliwaangalia ndugu zake wakubwa wakienda katika darasa la Wasichana na Wavulana.

Picha
alt text

Pia aliona jinsi walivyokuwa na furaha walipokuwa wakienda hekaluni. Akoni pia alikuwa na shauku ya kutembelea hekaluni.

Akoni alijitayarisha kwa ajili ya darasa la Wavulana kwa kwenda kanisani na kuzungumza na familia yake.

Aliuliza maswali kuhusu hekalu ili awe tayari kuingia ndani.

Picha
alt text

“Nilikuwa na shauku kuingia hekaluni kwa mara ya kwanza,” anasema Akoni. “Lakini ninapokuwa hekaluni, najihisi niko salama.”

Picha
alt text

Hekalu la karibu na Akoni ni Hekalu la Albuquerque New Mexico. Liko umbali wa mwendo wa masaa manne. Akoni anafurahi kwamba hivi karibuni hekalu jipya litajengwa jirani zaidi.

Akoni anatumaini kuhudumu misheni siku moja, kama vile ndugu zake wakubwa.

Ameanza kushiriki injili kwa kumwalika rafiki yake aje kanisani. Anataka kuwa mfano kwa mdogo wake na wengine pia!

Picha
alt text

Miamba hii mirefu katika picha hii inaitwa “mabawa ya miamba.” Eneo hili ni muhimu kwa watu wa Navajo.

Picha
alt text here

Chapisha