2023
Kwenye Mstari, Kaa Tayari, Anza!
Novemba 2023


“Kwenye Mstari, Kaa Tayari, Anza!” Liahona, Nov. 2023, 38.

Kitu cha kuburudisha

Kwenye Mstari, Kaa Tayari, Anza!

Picha
alt text here

Vielelezo na Colleen Madden

Hapa kuna baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kukusaidia ujiandae kwa ajili ya Wasichana au Wavulana. Je, unaweza kupata mambo manne yanayofuatana?

  • Weka alama kwenye maandiko yako.

  • Zungumza na mtu ambaye yawezekana ana wasiwasi kuhusu kuhama kutoka darasa la Msingi.

  • Ning’iniza juu nyumbani andiko unalolipenda.

  • Shiriki ushuhuda wako na mtu.

  • Mwombe askofu wako au rais wa tawi nakala yako ya Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi.

  • Pamba daftari la kwenda nalo darasani.

  • Nafasi ya Wazi

  • Andika ujumbe wa shukrani kwa mwalimu wa Msingi

  • Soma maswali ya usaili wa kibali cha hekaluni. (Unaweza kuyapata katika ( ukurasa wa 37 wa gazeti la Rafiki la mwezi Novemba 2022.)

  • Mwulize mtu kuhusu darasa la Wavulana au Wasichana likoje.

  • Mwombe mshiriki wa darasa lako aende na wewe kwenye darasa lako jipya.

  • Andika matarajio yako katika darasa la Wasichana au Wavulana.

  • Kutana na kiongozi kutoka kwa Wasichana au Wavulana.

  • Andika mambo mawili unayotaka kujifunza katika darasa la Wasichana au Wavulana.

  • Soma makala katika gazeti la Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana.

  • Mwulize kiongozi wako mpya kuhusu shughuli za darasa. Ziandike kwenye kalenda yako!

Chapisha