Shughuli za “Njoo, Unifuate kwa ajili ya Watoto Wadogo,” Rafiki, Nov. 2023, 49.
Shughuli za Njoo, Unifuate kwa ajili ya Watoto Wadogo
Kwa ajili ya Waebrania 1–6
Jifanye mnasafiri pamoja kwa meli. Je, utajuaje mahali pa kwenda? Zungumza kuhusu jinsi gani Yesu Kristo ni kama nahodha (ona Waebrania 2:10). Tunapomwamini Yeye, anaweza kutuongoza kwa usalama katika maisha yetu.
Kwa ajili ya Waebrania 7–13
Imbeni “Faith,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97). Zungumza kuhusu jinsi sisi tunavyoonesha imani yetu pale tunapomtumaini Mungu na kumfuata Yesu Kristo.
Kwa ajili ya Yakobo
Tengenezeni kiburudisho pamoja. Wakati kinapikwa, uliza, “je, ni vigumu kusubiri?” Kusubiri siyo rahisi. Lakini tunaposubiri mambo mazuri huja—kama baraka za Mungu—daima zinastahili kusubiriwa.
Kwa ajili ya 1 na 2 Petro
Watoe watoto wako nje ya chumba. Je, ni siku ya jua kali? Siku ya mvua? Fikiria kitu unachoweza kufanya ili kufurahia hali ya hewa. Fundisha kwamba tunaweza kuwa na furaha, bila kujali mambo yanayotuzunguka.
Kwa ajili ya 1–3 Yohana; Yuda
Pima jinsi gani watoto wako wadogo walivyo warefu. Fundisha kwamba kadiri Yesu alivyokuwa anakua, alikuwa akifanya chaguzi njema kila siku. Waombe wataje ni uchaguzi gani mzuri walioufanya leo. Wasaidie waseme, “Mimi ninakua, kama Yesu alivyokuwa!”