2023
Yesu Kristo Alimponya Mtu
Novemba 2023


“Yesu Kristo Alimponya Mtu,” Rafiki, Nov. 2023, 24–25.

Hadithi za Yesu

Yesu Kristo Alimponya Mtu

Ondoa ukurasa huu na ukunje katika nusu mbili zinazolingana. Kisha inua picha juu wakati ukisimulia hadithi.

Picha
alt text here

Kielelezo na Sam Lawlor

Siku moja, Yesu alimwona mtu aliyekuwa kipofu. Baadhi ya watu walifikiri Mungu amemfanya kuwa kipofu ili kumwadhibu. “Je, mtu huyu alitenda dhambi? Au wazazi wake walitenda dhambi?” waliuliza.

Yesu alisema upofu wa mtu yule haukuwa adhabu. “Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake,” Alisema.

Yesu aliweka tope juu ya macho ya mtu yule. Kisha akamwambia mtu yule aende kunawa kwenye birika la maji. Mtu yule alipofanya kile Yesu alichosema, aliponywa. Mtu huyo aliweza kuona.

Nyakati zingine mambo magumu hutokea kwetu. Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni wanaweza kutusaidia sisi tujifunze, tukue na tuwe na amani. Wao wanatupenda sisi na wanataka kutubariki!

Chapisha