“Miuhtasari wa Mkutano,” Rafiki, Mei 2023, 5.
Miuhtasari ya Mkutano
Msaada kutoka kwa Roho Mtakatifu
Rais Eyring alisema kwamba yeye anahisi kutiwa moyo wakati anaposoma hadithi ya Nefi akiyachukua mabamba ya shaba kutoka kwa Labani. Nefi hakujua hasa cha kufanya, lakini yeye aliongozwa kila dakika na Roho Mtakatifu. Wakati Bwana anapotutaka tufanye jambo gumu, Roho Mtakatifu atatusaidia pia.
Hii inanifundisha:
Kumbuka Wewe U Nani
Mzee Stevenson alitualika sisi tusimame kila wakati tunapojiona wenyewe kwenye kioo na kusema, “Wee, hebu nitazame! Mimi ni wa kupendeza! Mimi ni mwana wa Mungu, Yeye ananijua! Yeye ananipenda!” Kufanya hivi kutatusaidia kukumbuka sisi ni kina nani kweli na jinsi gani Mungu na Roho Mtakatifu wanaweza kutusaidia.
Hii inanifundisha:
Imani katika Yesu Kristo
Mzee Costa alishiriki hadithi ya wakati ambapo Yesu Kristo alituliza dhoruba. Sisi sote tunazo dhoruba, au changamoto, katika maisha ambazo ni ngumu. Lakini kamwe hatutakabiliana nazo peke yetu. Kuwa na imani katika Yesu Kristo kunatupatia sisi nguvu na amani tunayohitaji ili kukabiliana na dhoruba yo yote.
Hii inanifundisha:
Kutembea katika Njia pamoja Naye
Rais Freeman alisimulia hadithi kuhusu wakati yeye alipoenda kutembea kwenye njia maalum, licha ya kuwa alikuwa ameumia kiwiko chake cha mguu. Hangeweza kutembea kwenye njia ile peke yake, kwa hiyo mwongozaji wa nja ile alimsaidia. Kama vile mwongozaji wa Rais Freeman, Yesu Kristo atatusaidia katika changamoto yo yote kama tunajitahidi kushika maagano yetu.
Hii inanifundisha: