2023
Habari za Mkutano
Novemba 2023


“Habari za Mkutano,” Rafiki, Nov 2023, 4.

Habari za Mkutano

Nukuu za Mkutano

Kutazama Mkutano Mkuu kote Ulimwenguni

Picha
Msichana mwenye tabasamu

Kwa sababu ya tofauti ya muda, tunatazama vikao vya asubuhi vya mkutano mkuu wakati wa jioni. Sisi tulisisimka wakati Rais Nelson alipotangaza mahekalu mapya!

Sofia D., umri miaka 11, Mkoa wa Bratislava, Slovakia

Picha
Msichana mwenye tabasamu

Tunajiandaa kwa ajili ya mkutano mkuu kwa kuenda kununua vitafunwa na kupumzika ili tusisinzie katikati ya mkutano. Tunasali kama familia kwa ajili ya uelewa na kusoma maandiko. Mimi daima ninasisimka kusikiliza nabii aliye hai na kusikia neno la Mungu.

Runakorwashe S., umri miaka 7, Mkoa wa Kusini, Malawi

Picha
Mvulana mwenye kutabasamu

Kutazama mkutano mkuu kumenifanya nitake kuwa karibu na Yesu Kristo. Yeye ndiye Mchungaji Mwema, na Yeye anatujali sisi, kondoo Wake. Wakati mwingine tunachepuka kidogo, lakini Yeye daima huja kututafuta sisi.

Efrain C., umri miaka 9, San Juan Province, Argentina

Mahekalu 20!

Kulikuwa na mahekalu mapya 20 yaliyotangazwa katika mkutano mkuu! Tumia ramani ili kupata eneo la kila hekalu jipya. Paka rangi kwenye sehemu katika umbo la hekalu unapolipata kila moja.

Savai’i, Samoa

Cancún, Mexico

Piura, Peru

Huancayo, Peru

Viña del Mar, Chile

Goiânia, Brazil

João Pessoa, Brazil

Calabar, Nigeria

Cape Coast, Ghana

Luanda, Angola

Mbuji-Mayi, Democratic Republic of the Congo

Laoag, Philippines

Osaka, Japan

Kahului, Hawaii, USA

Fairbanks, Alaska, USA

Vancouver, Washington, USA

Colorado Springs, Colorado, USA

Tulsa, Oklahoma, USA

Roanoke, Virginia, USA

Ulaanbaatar, Mongolia

Zaka na Matoleo

Katika mkutano mkuu, tumejifunza baadhi ya njia Kanisa hutumia fedha zetu za zaka na michango ili kuwabariki watu kote duniani!

  • Mwaka jana, zaidi ya dola bilioni 1 za Marekani zilitumika kuwabariki wale walio na uhitaji.

  • Dola milioni 54 zingine ziliwasaidia akina mama na watoto walio na uhitaji.

  • Zaka husaidia kuwakimu zaidi ya wamisionari 71,000 waotumikia katika misheni 414 .

  • Zaka pia husaidia kutunza mikusanyiko 30,000 katika nchi na maeneo 195.

Masomo ya Maisha kutoka kwa Nabii

Rais Nelson amefika umri wa miaka 99 mwaka huu! Katika hotuba yake, alishiriki baadhi ya masomo ambayo yeye alijifunza katika karibia miaka 100 ya maisha. Nenda ukurasa wa 2 ili kusoma kitu ambacho alifundisha.

Picha
PDF ya hadithi

Chapisha