2023
Salamu kutoka Indonesia
Novemba 2023


“Salamu kutoka Indonesia!” (Rafiki, Nov. 2023, 18–19).

Salamu kutoka Indonesia!

Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni ulimwenguni kote.

Picha
alt text here

Indonesia ni nchi iliyopo Kusini Mashariki mwa bara la Asia. Ina visiwa zaidi ya 17,000! Takribani watu milioni 280 wanaishi huko.

Kanisa Linalokua

Picha
alt text here

Rais Russell M. Nelson aliwatembelea waumini katika mji mkuu, Jakarta, mwaka 2019. Na katika mkutano mkuu wa Aprili 2019, alitangaza kwamba hekalu lingejengwa huko!

Mahali pa Kuabudu

Picha
alt text here

Indonesia ina msikiti mkubwa wa Kiislamu kuliko yote iliyoko Kusini Mashariki mwa Asia. Ina hekelu la Kibudha kubwa zaidi ulimwenguni.

Volkano ya Bluu!

Picha
alt text here

Indonesia inazo volkano hai nyingi kuliko nchi nyingine yoyote. Volkano ya Kawah Ijen ina miale ya rangi ya bluu ambayo inaweza kuonekana usiku.

Je, Wewe Unazungumza Lugha Yangu?

Picha
alt text here

Kiindonesia ni lugha rasmi. Zaidi ya lugha 700 huzungumzwa huko Indonesia. Kauli mbiu ya nchi yao inamaanisha “Wengi, lakini mmoja” ili kuonesha kwamba ni wamoja.

Nyumba ya Majoka

Picha
alt text here

Majoka wa Komodo ndio mijusi wakubwa zaidi ulimwenguni. Wanaweza kukua hadi kuwa urefu wa futi 10 (mita 3)!

Picha
alt text here

Vielelezo na Conner Gillette

Chapisha