2022
Eneo la Kati la Afrika Linamuaga Mzee Joseph na Dada Gladys Sitati
Septemba 2022


Maoni ya Mhariri

Eneo la Kati la Afrika Linamuaga Mzee Joseph na Dada Gladys Sitati

Eneo la Kati la Afrika linatoa shukrani zake za dhati kwa Mzee Joseph W. Sitati na Dada Gladys Sitati kwa huduma yao katika eneo. Mzee Sitati alihudumu kama Rais wa Eneo la Kati la Afrika tangu Agosti 2020 hadi Agosti 2022, akisaidiwa na mkewe Gladys.

Mzee Sitati aliidhinishwa kama Sabini Mkuu Mwenye Mamlaka wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho mnamo 2009 na ametumia miaka 13 iliyopita akihudumu kwa uaminifu katika nafasi tofauti tofauti, ikiwa ni pamoja na kama Mshauri katika Urais wa Eneo la Magharibi la Afrika, mkurugenzi mtendaji msaidizi katika Idara ya Ukuhani na Familia, mkurugenzi mtendaji msaidizi katika Idara ya Umisionari na Mshauri wa Kwanza katika Eneo la Kusini Mashariki la Afrika. Sasa amepumzishwa kwa heshima kama kiongozi mkuu mwenye mamlaka na anatambulika kama sabini anayeshikilia cheo chake.

Wanaposonga kuelekea hatua hii mpya ya maisha yao, tunaomba kwamba akina Sitati waweze kubarikiwa kwa wingi kwa uongozi na huduma yao iliyotolewa kwa moyo wa dhati.