Habari za Eneo
Brazzaville: ‘Imani yetu haijawa kamilifu, lakini Bwana alitukumbuka’
Watakatifu huko Jamhuri ya Kongo wanafurahia habari ya shangwe kwamba kutakuwa na hekalu litakalojengwa katika nchi yao.
Mnamo Aprili 3, 2022, watakatifu waaminifu kote ulimwenguni walikusanyika katika nyumba zao kutazama Mkutano Mkuu. Huko Jamhuri ya Kongo, Brazzaville Rais wa Kigingi Belle-Vie Gayouele pamoja na familia yake walikuwa kati ya mamilioni ya watakatifu wakiweka hema zao kuelekea Kituo cha Mikutano wakati kwa unyenyekevu walipofuatilia mkutano kupitia matangazo ya moja kwa moja, pale Rais Russell M. Nelson alipotangaza kwamba hekalu litajengwa Brazzaville!
Juu ya uzoefu huu mtakatifu, Rais Belle-vie Gayouele anasema, “Hatukutarajia kabisa hekalu kutangazwa kwenye mkutano huu wa hivi karibuni. Hata hivyo, watakatifu kote Brazzaville na Pointe-Noire (miji miwili ndani ya nchi) walifuatilia maneno ya Nabii ya kutamatisha kwa nuru ya tumaini. Wakati nabii bila kutarajiwa alipotangaza ujenzi wa hekalu Brazzaville, ilikuwa na matokeo ya kustaajabisha. Mke wangu, kwa mfano, alilia kwa shangwe, kulikuwa na shamra shamra kubwa kila mahali, video zisizokoma na simu na usiku huo hatukuweza kulala! Mimi na familia yangu tulipiga magoti kwa unyenyekevu na kutoa sala ya shukrani.”
Dada Estelle Vianney, mshiriki wa Kata ya Massa Kigingi cha Brazzaville, anasema kwamba amejawa na shukrani. “Leo nina shukrani kubwa kwamba Baba yetu wa Mbinguni ametangaza kupitia Nabii aliye hai habari kuu kwamba nyumba yake itajengwa kwenye nchi yangu,” alisema. “Nimehisi kwamba hakika Bwana anatufahamu na anatukumbuka sisi, Watakatifu wa Brazzaville. Moyo wangu umejawa shangwe.” Hisia sawa na hizo zilikuwa kwa wote Dada Bibicha Kitombo wa kata ya Mpaka 1st, Kigingi cha Pontre-Noitre na Kaka Van Sambala wa Kata ya Aeroport Kigingi cha Aeroport wakithibitisha kwamba mioyo ya Watakatifu imeunganika pamoja katika umoja na katika upendo.
““Leo hapa Brazzaville, kuna aina ya furaha kwenye nyuso za waumini, kuridhika. Unaweza kwa hakika kuhisi, amani ya kina na msimamo wa hali ya juu kwenye ibada za hekalu, baadhi ya watu bado hawaamini, shangwe ni kuu na shukrani kwa ajili ya wema wa Bwana ni ya kina,” anasema Rais Belle-Vie Gayouele.
Hekalu la karibu kwa watakatifu wa Brazzaville kwa sasa liko Kinshasa, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Kufika huko mara nyingi imekuwa si rahisi.
“Tulipanga safari kubwa ya hekaluni huko Kinshasa, ambayo ilimaanisha kuwa tulipaswa kuvaa ujasiri wa changamoto ya kuvuka mto unaotiririka kwa kasi tukiwa na familia zetu,” anasema Rais Belle-Vie Gayouele. “Ilikuwa pia wakati ambapo nchi yetu ilikuwa ikipitia mdororo mkubwa wa uchumi. Familia zilikuwa na dhiki, lakini kwa safari hizi, waumini walifanya dhabihu kubwa, kulipia tiketi kwa ajili ya kuvuka mto, chakula na malazi. Kulikwepo wengi wetu tuliokuwa tukienda hekaluni kiasi kwamba mara nyingi hakukuwa na nafasi ya kutosha kwa ajili yetu katika hekalu la kinshasa. Baadhi ya akina kaka na akina dada walilazimika kubaki nje ya hekalu na kusubiri zamu yao. Safari hizi zilikuwa nyakati za jaribu la imani na msimamo kwenye ibada za hekaluni. Hatimaye, safari hizi zimetuwezesha kumleta Roho wa hekalu ndani ya mioyo ya waumini wa Kanisa,” anasema.
Dada Bibicha Kitombo anaongeza, “Viongozi wamekuwa chanzo kikuu cha msaada na kutia moyo, hasa kwa vijana na vijana wadogo waseja kwa kuwatia moyo ili wafokasi kwenye hekalu. Van Sambala anashiriki kwamba hili limemwezesha kusali, kufunga mara kwa mara na kuwa imara katika kutii maagano.”
Dada Estelle Vianney anawakumbusha watakatifu kwamba kila mtakatifu anapaswa kujiandaa sasa ili kupokea baraka za hekaluni. Anashiriki nukuu kutoka kwa Rais Richard G. Scott ambayo inasema, “ustahiki binafsi ni sharti muhimu la kupata baraka za hekaluni”.1 Ushuhuda wake ni rahisi: hekalu ni Nyumba ya Mungu, ni msingi wa kuimarisha imani na uthabiti wa kiroho.
Rais Belle-Vie Gayouele anashauri: “Leo tunajua kwamba imani yetu haijawa kamilifu, juhudi na dhabihu zetu hazijawa kubwa, lakini tuna shukrani kwamba Bwana ametukumbuka.
“Hekalu litabariki nchi hii na watu, wote waumini na wasio waumini. Hekalu hili litakuwa baraka kwetu sisi na watoto wetu. Kanisa litatoka kusikoonekana na litaleta Roho wa Mungu kwa wingi kwenye nchi yetu.”