Msaada Kidogo wa Ziada
Mifupa ya Dinosau ilionekana kufurahisha sana kuliko tiba ya uwezo wa kuongea.
“Alex, ni wakati wa kwenda kwenye tiba ya uwezo wa kuongea,” Bi. Jenkins alisema.
Alex aliinamisha kichwa chake. Tiba ya uwezo wa kuongea ni darasa la kipekee alilowahi kwenda. Alikuwa na tatizo kusema baadhi ya maneno na sauti. Hivyo alihitaji kufanyia mazoezi vitu hivyo katika darasa la uwezo wa kusema mara kadhaa kwa wiki. Kila wakati alipomaliza darasa lake la kawaida, aliondoka akijihisi kuaibika!
Alimwangalia mwalimu wake. “Ninaweza kuliruka hili kwa leo?” alinong’ona. “Kwa leo tu?”
Leo, Bwana Timmons alikuwa anakuja darasani kwa Alex kuzungumza kuhusu Dinosau. Bwana Timmons alikuwa akifanya kazi katika Makumbusho ya vitu vya kale yenye mifupa mingi mizuri ya Dinosau. Alikuwa pia analeta mfupa ambao una umri wa maelfu ya miaka! Alex hakutaka kukosa hayo.
Bi. Jenkins akatabasamu. “Wewe bado unahitaji kwenda kwenye darasa lako la uwezo wa kuongea. Lakini unaweza kurudi kwa wakati kwa ajili ya sehemu ya mwisho ya mazungumzo ya Bwana Timmons.”
Alex alijaribu kurudisha tabasamu, lakini hakuweza. Pole pole alitembea kuelekea kwenye darasa la tiba ya uwezo wa kuongea. Darasani walifanyia mazoezi kutamka sauti ile ile tena na tena. Kujifunza kuhusu dinosau ingekuwa ya kuburudisha zaidi.
“Ninachukia kusema sauti hizi za kijinga,” alimwambia mwalimu wake wa tiba ya uwezo wa kuongea. “Najihisi kama mtoto.”
“Wewe sio mtoto kabisa,” mwalimu alisema. “Sisi sote tunahitaji msaada kidogo wa ziada wakati mwingine. Ulijua kwamba mimi nilienda kwenye tiba ya uwezo wa kuongea nilipokuwa umri wako?”
Hilo lilimfanya Alex ajihisi vizuri kidogo. Alifanya kazi kwa bidii kwa sehemu yote iliyobaki ya darasa la mazoezi ya sauti yake.
Aliporudi kwenye darasa la Bi. Jenkins, alimwona rafiki yake Courtney akiondoka.
“Unaenda wapi?” aliuliza.
Courtney alitazama chini. “Ninapata matatizo katika kusoma. Nahitaji kwenda katika darasa maalumu la kusoma.” Courtney alionekana kuhisi kuaibika.
“Hapana, ni sawa tu” Alex alisema. “Mimi ndiyo nimerudi tu kutoka kwenye darasa langu la uwezo wa kuongea. Nimetumia muda wote kufanya sauti hiyo hiyo tena na tena. Alipangusa pua yake.
“Umefanya?”
Aliitikia kwa kichwa. “Nimekuwa nikienda kwenye tiba ya uwezo wa kuongea kwa miaka miwili iliyopita.”
“Imekuwaje sikuwa nikijua hilo?” Courtney aliuliza.
Alex alijibu kwa kupandisha mabega. “Sikuwahi kumwambia mtu yeyote. Niliogopa watu wangenifanyia mzaha.”
“Kamwe nisingekufanyia mzaha,” Courtney alisema. “Nimefurahi kuwa umerudi katika wakati muafaka kuona mfupa wa dinosau. Ni safi sana!” Courtney alimpungia mkono “Nahitaji kuondoka. Tutaonana baadaye.”
Punde Alex aligundua kwamba yeye na Courtney hawakuwa watu pekee waliokuwa wakienda kwenye madarasa mengine. Tommy alienda kwenye darasa la kumsaidia kujifunza vyema maarifa ya jamii. Na Beka alifanya kazi na mwalimu maalumu ili kumsaidia mkono wake uimarike baada ya kuumia.
Sasa Alex hakujihisi vibaya sana kuhusu darasa lake la uwezo wa kuongea. Alitaka kuwasaidia watoto wengine nao wahisi vizuri pia. Alifanya mazoezi ya kusoma pamoja na Courtney na alizungumza na Tommy wakati wa chakula cha mchana. Kila mtu alihitaji msaada kidogo wa ziada wakati mwingine, na hilo ni SAWA.