WAANZILISHI katika Kila Nchi
Felipe Anaipata Njia
“Tafadhali tusaidie tuipate njia yetu,” Felipe alisali.
Felipe alijua kuwa jua linazama. Ndege wameacha kuimba, na nyenje walikuwa wakilia kwa sauti zaidi. Yeye na mama yake walikuwa wametembea msituni kwa zaidi ya saa mbili. Lakini kila njia waliyoiendea ilionekana kuwa kama ile ya mwisho. Walikuwa wamepotea kabisa.
Felipe alielekea kuogopa kabisa. Ni kwa muda gani wangeweza kubaki salama mle msituni? Alikuwa na umri wa miaka 10 tu. Huo haukuwa umri wa kutosha kupambana na nyoka au nguruwe mwitu. Na viumbe gani wengine wa kutisha yawezekana wakawa katika kuwinda baada ya jua kuzama? Wazo hili lilipeleka mzizimo kwenye uti wake wa mgongo
Kuwa jasiri, alijiambia mwenyewe. Alijua alitakiwa kuwa hivyo.
Felipe alitamani baba yake angelikuwa hapo. Lakini alikuwa amefariki miezi sita iliyopita. Bila yeye, mambo yalikuwa magumu kwa Felipe na mama yake. Walikuwa wameishiwa pesa na chakula.
Felipe alitumaini wangeweza kufika nyumbani kwa dada yake upande mwingine wa mlima mapema. Yeye angeweza kuwapa pesa za kununua mchele.
Alisema sala moyoni mwake. “Baba wa Mbinguni, tafadhali tusaidie kuipata njia yetu. Tafadhali.”
Kisha wazo likamjia: Angalia minazi. Felipe akatazama juu. Ile, kwa mbali, kulikuwa na kisitu cha miti ya minazi. Aliweza kuiona juu kabisa ya miti mingine humo porini. Majani yake yalikuwa yakipunga kwenye upepo. Kwa mara ya kwanza baada ya saa nyingi, Felipe akahisi matumaini.
“Tazama!” Yeye alionyesha kwenye ile miti.
Mama yake akaelewa. Minazi ilimaanisha kijiji kiko karibu. Mungu alikuwa amejibu sala ya Felipe. Felipe aliushika mkono wa mama yake. Kwa pamoja walitembea kwenye usalama wakati jua lilipozama.
Felipe daima alikumbuka jinsi Mungu alivyojibu sala yake. Nyakati zingine alitamani kuweza kusikia sauti ya Mungu vyema zaidi kama alivyosikia usiku ule pale msituni.
Kisha siku moja, miaka minane baadaye, Felipe alikutana na wamisionari. Walikuwa wanatokea Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Walimfundisha kuhusu manabii wanaoishi, ambao walinena maneno ya Mungu. Hili ndilo lile Felipe alilokuwa akilitumaini!
Felipe alihamasika kujiunga na Kanisa. Alikuja kuwa mmoja wa wamisionari wa kwanza kutoka Ufilipino kushiriki injili huko. Tena, Mungu alikuwa amemwonyesha Felipe mahali pa kwenda—na Felipe alijua daima Mungu angefanya hivyo.