2022
Kutana na Carmen kutoka Lebanoni
Novemba 2022


Mikono ya Usaidizi Ulimwenguni Kote

Kutana na Carmen kutoka Lebanoni

Kutana na watoto wa Msingi wakiwasaidia wengine, kama Yesu alivyofanya.

A young girl named Carmen Ahmad stands outside and smiles.

Yote kuhusu Carmen

Carmen Ahmad with her three older siblings.

Umri: miaka 8

Kutoka: Syria lakini sasa anaishi Lebanoni

Lugha: Kiarabu, Kingereza

Malengo na ndoto: 1) Kutembelea hekalu. 2) Kuwa msanii. 3) Kutumikia misheni.

Familia: Carmen anao dada wawili wakubwa na kaka mmoja mkubwa.

Mikono Saidizi ya Carmen

Carmen Ahmad smiles with a box full of supplies.

Carmen na mama yake wanaishi huko Lebanoni, lakini walikuwa wakiishi huko Syria. Majirani zao wanatokea Syria pia. Desemba iliyopita, Carmen alitaka kufanya kitu cha ukarimu kwa ajili yao. Kila siku hadi Krismasi, Carmen alinunua kitu kimoja kidogo kutoka dukani. Aliviweka vyote kwenye boksi. Baada ya siku 25, boksi lilikuwa limejaa. Siku ya Krismasi, Carmen alilichukua lile boksi na kulipeleka kwa majirani zake. Walishukuru sana. Carmen anasema huduma yake ilimsaidia yeye kukumbuka huduma ambayo Yesu Kristo aliitoa. “Tunapoonyesha upendo kwa wengine,” Carmen anasema, “sisi tunauhisi upendo wa Mungu.”

Mambo Pendwa ya Carmen

Mahali: Ufukweni

Hadithi kuhusu Yesu: Wakati Yesu alipotembea juu ya maji

Wimbo wa Msingi: “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 228–29)

Chakula: Tambi, aiskrimu ya matunda

Rangi: Zambarau isiyokolea

Somo shuleni: Sayansi

story PDF

Vielelezo na Svetla Radivoeva