2022
Maongezi na Xiomara kuhusu Kuwa Mpya katika Kikundi cha Wasichana
Novemba 2022


Maongezi na Xiomara kuhusu Kuwa Mpya katika kikundi cha Wasichana.

Xiomara (inatamkwa she-o-MA-ra) ni kutoka Chiapas, ni jimbo huko Mexico kusini. Amehamia hivi karibuni katika kikundi cha Wasichana.

Picha
Illustration of Xiomara.

Kwanza, tunataka tukujue.

Unafanya nini kwa ajili ya kujiburudisha?

Naendesha baiskeli yangu, nacheza soka na kupika. Pendeleo langu la kitu cha kupika ni quesadillas!

Je, unapenda rangi gani?

Manjano.

Ni kitu gani ulikitazamia zaidi kuhusu kuhama kwako kutoka Msingi kuja kwa Wasichana.

Nilikuwa na shauku kubwa ya kwenda hekaluni na kufanya ubatizo.

Je, ulihisije kuhusu kwenda kikundi cha Wasichana kwa mara ya kwanza?

Mara ya kwanza ilikuwa vigumu. Nilikuwa na hofu kuhusu wasichana wakubwa wangefikiri nini kuhusu mimi. Nilikuwa na wasiwasi kidogo hadi pale wote tulipoenda hekaluni kwa pamoja. Hapo ndipo tulipokuja kuwa marafiki wazuri.

Je, ilikuwaje kwenda hekaluni kwa mara ya kwanza?

Picha
Xiomara walking in front of the Tuxtla Gutierrez Mexico Temple.

Ilikuwa siku maalumu sana. Kuingia ndani ya hekalu la Bwana lilikuwa tukio la kiroho. Daima nimekuwa nikitaka kwenda hekaluni. Katika Msingi tuliimba, “Napenda kuona hekalu. Nitaenda huko siku moja.” Sasa naweza kusema, “Napenda kwenda hekaluni.”

Mara hiyo ya kwanza hekaluni, nilifanya ubatizo kwa baadhi ya mashangazi zangu, baadhi ya ndugu wa bibi yangu (mama wa mama yangu) na watu wengine nisiowajua. Hekalu na historia ya familia ni sehemu ya ushuhuda wangu.

Ni shughuli gani za burudani umefanya pamoja na kikundi chako cha Wasichana?

Picha
A batch of chocolate chip cookies.

Kutengeneza biskuti! Tulitengeneza biskuti 150. Halafu tukala pamoja na watu wengine. Shughuli za Wasichana zinaburudisha. Zimejaa masomo mazuri, uhamasishaji na mwongozo ili kutusaidia kuwa wamisionari wa baadaye.

Je, kuna wasichana wengine wa umri wako katika kata yako?

Ni mimi tu. Pia huko shuleni mimi ni muumini pekee wa Kanisa katika darasa langu.

Je, ni vigumu kuwa muumini pekee wa Kanisa shuleni?

Hapana. Marafiki zangu wote wanajua kuwa mimi nafuata dini tofauti na wao, lakini hawanitendei lolote la tofauti.

Je, nini unakipenda zaidi kuhusu kuwa katika kikundi cha Wasichana?

Napenda kujifunza zaidi kuhusu Mwokozi na mpango wa wokovu. Ni baraka kubwa kufanya kazi ya historia ya familia. Napenda kufanya ubatizo ili kuwapatia matumaini ndugu zangu ambao tayari wameiaga dunia hii.

Napenda kuwa katika programu ya Wasichana!

Picha
story PDF

Vielelezo na Alyssa Tallent

Chapisha