2022
Fokasi kwenye Hekalu
Novemba 2022


“Fokasi kwenye Hekalu,” Rafiki, Novemba 2022, 2–3.

Ujumbe wa Mkutano kutoka kwa Nabii

Fokasi kwenye Hekalu

Imetoholewa kutoka “Fokasi kwenye Hekalu,” Liahona, Nov. 2022.

ujumbe kuhusu hekalu

Kielelezo cha Hekalu na Bailey Rees; ukurasa wa kupaka rangi na Bryan Beach

Hivi karibuni, Mimi pamoja na Dada Nelson tuliangalia video mpya za Kitabu cha Mormoni. Mojawapo ya video hizi ilimuonesha Mwokozi akiwatokea Wanefi. Alisema,“Tazama, mimi ni Yesu Kristo… Mimi ndimi nuru na uzima wa ulimwengu” (3 Nefi 11:10–11).

Ni muhimu kwamba Mwokozi aliwatokea watu kwenye hekalu. Ni nyumba Yake. Imejawa nguvu Zake.

Bwana anaharakisha ujenzi wa mahekalu. Anafanya hivyo ili watu wengi waweze kwenda hekaluni. Ninaahidi kwamba kuhudhuria hekaluni mara kwa mara kutawabariki watu katika njia ambazo hakuna chochote kingine kinachoweza.

Katika mkutano, nilitangaza mahekalu mengine zaidi 18. Katika baadhi ya miji mikubwa, inachukua muda mrefu kwa watu kusafiri kwenda hekaluni kwenye miji yao. Kwa hiyo tunakwenda kujenga mahekalu mengine katika baadhi ya miji hii mikubwa. Manne kati ya mahekalu mapya yatajengwa karibu na Jiji la Mexico.

Wapendwa akina kaka na dada zangu, na muendelee kufokasi kwenye hekalu zaidi kuliko mlivyowahi kufanya hapo kabla. Ninawabariki ili mzidi kusogea karibu na Mugu na Yesu Kristo kila siku. Ninawapenda. Mungu awe nanyi mpaka tutakapokutana tena.

Yesu Aliwatembelea Wanefi

ukurasa wa kupaka rangi wa Yesu akiwatokea Wanefi

Mwokozi aliwatokea Wanefi katika hekalu kwa sababu ni nyumba Yake. Mungu hutubariki kwa mahekalu zaidi ili kutuimarisha na kutulinda.