Salamu kutoka Lebanoni!
Ungana na Margo na Paolo wanaposafiri kuzunguka ulimwengu ili kujifunza kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni.
Lebanoni iko Mashariki ya Kati. Takribani watu milioni 7 wanaishi huko.
Majiji ya Pwani
Mpaka wote wa magharibi wa Lebanoni unagusa Bahari ya Mediterania. Wasichana hawa wako kwenye ufuko wa bahari katika mji mkuu, Beiruti.
Lugha Rasmi
Hiki ni kitabu cha Mafundisho na Maagano kwa Kiarabu, lugha rasmi ya Lebanoni.
Tabbouleh
Saladi hii imetengenezwa kwa kitimiri, nyanya, nanaa, kitunguu na bulga (aina ya nafaka).
Miseda ya Lebanoni
Wakati mmoja Lebanoni ilikuwa na miti mingi sana ya miseda. Miseda ya Lebanoni imetajwa zaidi ya mara 70 katika Biblia! Leo, bendera ya Lebanoni ina mti wa mseda juu yake.
Dini Mbili
Uislamu na Ukristo ndizo dini kuu za Lebanoni. Msikiti huu wa Kiislamu unasimama pembeni ya kanisa la Kikristo.