2022
Kitabu Maalumu
Novemba 2022


Kitabu Maalum

Picha
Border art from the Book of Mormon Stories surrounds Bernice (about age 5) who is holding the book. Her head pops out of the cover. Her parents are in the background.

“Baba, ni zamu yako kusoma,” Bernice alisema. Akafungua maandiko yake. Maman (Mama) na Baba walikaa karibu naye kwenye sofa.

Baba alisoma andiko la kwanza. “Ninajua kwamba anawapenda watoto wake.”

“Ninajua kwamba anawapenda watoto wake,” Bernice akarudia.

“Walakini,” Baba alisema, “sijui maana ya vitu vyote.”*

Walakini lilikuwa neno gumu. Bernice asingeweza kulisoma bado, na hakujua kile maneno yote yalichomaanisha. Lakini alipenda kuyarudia maneno hayo wakati familia yake iliposoma maandiko kwa pamoja.

Siku iliyofuata wakati wa maandiko, Baba alikuwa na jambo la kumshangaza. “Nina kitu maalumu kwa ajili yako,” Baba alisema. Akampatia Bernice kitabu. Kilikuwa na picha ya watu na boti kwenye jalada la mbele.

“Hiki ni kwa ajili yangu mimi?” Bernice aliuliza. Akakikumbatia kile kitabu kikubwa katika mikononi mwake.

“Kwa ajili yako,” Baba alisema. “Tazama ndani.”

Bernice alikifungua kile kitabu. Macho yake yakawa makubwa. Kulikuwa na picha nyingi za rangi.

“Kinaitwaje?” Bernice aliuliza.

Baba akayanyoshea kidole maneno juu ya jalada. “Hadithi za Kitabu cha Mormoni,” alisema.

Bernice alifuatilia maneno yale juu ya jalada. “Hadithi za Kitabu cha Mormoni,” alisema.

“Kina hadithi zile zile tunazozisoma katika maandiko,” Mama (Mama) alisema.

Bernice alielekeza kidole kwenye moja ya picha. “Huyo ni nani?” aliuliza.

“Hmm. Je, unaona upinde na mshale?” Maman aliuliza.

Bernice aliitikia kwa kichwa.

“Je, unakumbuka kusoma juu ya mtu fulani aliyekuwa na upinde uliovunjika?” Baba aliuliza.

“Nefi?” Bernice alisema.

“Ndio, huyo ni Nefi,” Baba alisema.

Bernice alitabasamu. “Asante, Baba. Asante, Mama. Ninakipenda kitabu hiki.”

Kila usiku, Bernice alisoma kitabu chake cha maandiko pamoja na Mama na Baba. Yeye alionyesha kwenye picha. Akajifunza kuyatamka baadhi ya maneno magumu. Na akajifunza kusoma baadhi ya maneno rahisi yeye mwenyewe.

Kusoma maandiko kulimfanya kuwa na furaha. Alifurahi kwamba aliweza kusoma pamoja na Mama na baba!

Chapisha