2022
Kibandiko cha shukrani
Novemba 2022


Kitu cha kuburudisha

Kibandiko cha shukrani

Picha
Page from the November 2022 The Friend Magazine.

Maandiko yanatufundisha kuwa na shukrani (ona Zaburi 100:4). Unaweza ukawa na burudani na ukawa mwenye shukrani unapocheza mchezo huu!

  1. Tafuta sehemu ya wazi ambako unaweza kukimbia. Chagua sehemu moja iwe “Eneo la Shukrani.”

  2. Kila mtu anaweza kumgusa mwingine! Unapokuwa umeguswa, weka mkono kwenye eneo uliloguswa. Unaweza bado ukawagusa watu kwa mkono wako mwingine

  3. Unapoguswa mara ya pili, weka mkono wako huo mwingine kwenye sehemu ya pili uliyoguswa.

  4. Unapokuwa umeguswa mara ya tatu nenda Eneo la Shukrani na sema vitu vitatu ambavyo unashukrani kwavyo. Utakapokuwa umekwishavitaja vitu vitatu, unaweza kujiunga na mchezo tena.

Kielelezo na Stefani McClary

Chapisha