“Onyesha na Elezea kutoka kwenye Mkutano,” Rafiki, Novemba 2022, 6–7.
Onyesha na Elezea kutoka kwenye Mkutano
Sophie, Bailey na Claire B., miaka 4, 8 na 6, kutoka Texas, Marekani, walitengeneza mahekalu kwa kutumia mchemraba wa sukari wakati wakisikiliza mkutano.
Fabiola R., miaka 12, kutoka Rio Grande do Sul, Brazil, hupenda kusikiliza mkutano pamoja na familia yake. Hawezi kusoma wala kuzungumza lakini huisi amani na upendo kutoka kwenye jumbe za mkutano. Sehemu anayoipenda sana ni kumsikiliza rafiki yake, Rais Henry B. Eyring.
Liesel L., miaka 9, Kansas, Marekani
Lucy M., miaka 7, Utah, Marekani
Milo M., miaka 8, Arizona, Marekani
Tunacheza mchezo wakati wa mkutano mkuu. Tunaweka kibandiko kwenye kipande cha karatasi kila mara tunaposikia jina la Kristo. Karatasi zetu huishia kujaa vibandiko!
Manu L., miaka 6, Tel Aviv, Israel
Napenda hadithi za kupendeza ambazo nabii na mitume hutuhadithia kuhusu maisha yao.
Adam L., miaka 9, Tel Aviv, Israel
Napenda muziki! Sehemu yangu pendwa ni kusikiliza kwaya ikiimba. Natumaini nitaimba kwenye kwaya siku moja.
Reuben F., miaka 4, Louisiana, Marekani
Napenda kumsikiliza nabii wetu na nyimbo maalumu za dini zinazoimbwa na Kwaya ya Tabenako.
Isaac E., miaka 6, Jimbo la Magharibi, Ghana
Napenda kuwa na familia yangu na kupaka rangi picha wakati wa mkutano mkuu.
William S., miaka 7, Tasmania, Australia
Napenda kumsikiliza nabii wetu na kusikia wapi mahekalu mapya yatajengwa.
Noah A., miaka 12, Al-Ahmadi, Kuwait
Tunapenda kusikiliza kwaya ikiimba na kufanya shughuli za mkutano.
Danielle, Hailey na Robin L., miaka 6, 10 na 9, Singapore