Shughuli za Njoo, Unifuate
Kwa ajili ya jioni ya nyumbani, kujifunza maandiko au hata kwa burudani tu.
Danieli na Tundu la Simba
Kwa ajili ya Daniel 1–6
Hadithi: Nabii Danieli aliomba dua kila siku. Watu wenye wivu walimtega mfalme katika kutengeneza sheria mbaya. Yeyote ambaye alisali kwa Mungu angetupwa kwenye tundu la simba! Hata hivyo Danieli aliendelea kusali. Alitupwa katika tundu la simba, lakini Mungu alimtuma malaika ili kumlinda. (Ona Daniel 6.)
Wimbo: “I Want to Live the Gospel” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 148)
Shughuli: Kata vikaragosi vya mikono kwenye ukurasa wa 17 na uvitumie kusimulia hadithi ya Danieli na tundu la Simba. Kwa nini ni vizuri kusali?
Yesu Alifufuka
Kwa ajili ya Hosea 1–6; 10–14; Yoeli
Hadithi: Hosea alikuwa nabii. Alifundisha kwamba Yesu Kristo angekufa na kufufuka. Hii ilifanyika ili sisi tuweze kuishi tena. (Ona Hosea 13:14.)
Wimbo: “Did Jesus Really Live Again?” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64)
Shughuli: Kwa sababu Yesu Kristo alifufuka, sisi sote tutaishi tena siku moja. Tafuta picha za washiriki wa familia ambao wamefariki. Simulia hadithi kuhusu wao.
Je, Nabii Alisema Nini?
Hadithi: Nabii Amosi alifundisha, “Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake” (Amosi 3:7). Hii inamaanisha kwamba Yesu Kristo anaongea na manabii Wake leo.
Wimbo: “We Thank Thee, O God, for a Prophet” (Nyimbo za Kanisa, na. 19)
Shughuli: Soma kile ambacho nabii amesema kwenye mkutano katika ukurasa wa 2. Alituambia nini? Chora picha kuonyesha vitu alivyofundisha.
Yona na Samaki Mkubwa
Hadithi: Bwana alimwita Yona ili akawafundishe watu wa Ninawi. Lakini Yona aliogopa. Alikimbia. Samaki mkubwa akammeza! Baada ya siku tatu akamtapika. Yona akatubu na akawafundisha wale watu. (Ona Yona 1–4).
Wimbo: “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11, mstari wa 7)
Shughuli: Nenda nje na tafuta mawe, majani au vijiti. Yatumie kutengeneza picha kuhusu Yona na samaki mkubwa.